Posts

JE UMEWAHI KUJUA UMUHIMU WA KUANDIKA WOSIA

Image
TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA Taratibu za kuandika wosia zinatofautiana kulingana na sheria ya mirathi inayotumika. 1. WOSIA WA MAANDISHI Wosia huu unashuhudiwa na watu wawili pale ambapo mtoa wosia anajua kusoma au kuandika. Shuhuda mmoja lazima awe ndugu wa karibu wa mtoa wosia na mwingine ambaye sio ndugu wa karibu.Wosia na unatakiwa uwe na tarehe, uandikwe kwa karamu ya wino au upigwe chapa na uwe na saini ya mtoa wosia na saini za mashuhuda ambapo wote wanatakiwa kutia saini zao kwa wakati mmoja. Mtoa wosia asiye jua kusoma ua kuandika awe na mashuhuda wa nne wanao jua kusoma na kuandika,muhusia huyo aweke alama ya kidole gumba cha mkono wake wa kulia,mashuhuda hao wote washuhudie na waweke saini zao kwenye Wosia kwa wakati mmoja. 2. WOSIA WA MDOMO/MATAMSHI Wosia huu unashuhudiwa na mashuhuda wasiopungua wa nne wawili kati yao ndugu wa mtoa wosia na wawili waliobaki wasio ndugu wa mtoa wosia.Wosia huu utolewa na mtu asiye jua kusoma na kuandika. TARATIBU ZA KUANDIKA WOSIA KATIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru Profesa Santishree Dhulipudi Pandit kwenye hafla iliyofanyika New Delhi nchini India Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru, New Delhi nchini India tarehe 10 Oktoba, 2023 Walimu wa Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru kilichopo New Delhi nchini India wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari wa Falsafa (Doctorate Honoris Causa) na Chuo hicho Oktoba 10, 2023 Wanafunzi wa Vyuo Vikuu mbalimbali nchini India wakiwa kwenye hafla ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alitunukiwa Shahada ya Heshim

KUWAJALI WATOTO YATIMA NA WALE WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI NI JUKUMU LETU SOTE KAMA JAMII. NEEMA GOSPEL CHOIR

Image
Katika dunia hii, tunahitaji kusimama pamoja na kuleta mabadiliko chanya. Tarehe 22 Julai 2023,   The Super Dom, Masaki ,  tunakuja na tukio la kipekee la chakula cha hisani linaloitwa "INSPIRE, EMPOWER, TRANSFORM for a Better  World" kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan,kulinda,kusaidia watoto yatima na wale wenye uhitaji maalumu wapo zaidi ya  Arobaini  waliotufikia kuomba msaada wa jamii  na kwa pamoja tumeamua kuushirikisha umma kujuika nasi, Watoto  h awa Wanahitaji upendo wetu, huduma yetu, na fursa ya kuwa na mustakabali mzuri. Kwa kujiunga nasi kwenye tukio hili, tunawapa tumaini la kuwa na maisha yaliyojaa furaha na mafanikio. Tutaimba,Pamoja tutawawezesha kwa Pamoja na tunakuomba popote ukiguswa Changia mchango wako kwa kutumia njia za malipo zifuatazo: Vodacom MPesa: 5922779, CRDB: 0133549137200, NMB: 20702302010. Amesisitiza Samuel Nkola. Mwenyekiti wa Neema Gospel Choir Neema Gospel Choir Na Mwandishi wetu. KUWAJ

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MAKAMU WA RAIS WA KAMPUNI YA KIMATAIFA YA PHILIP MORRIS GREGOIRE VERDEAUX IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Philip Morris, Gregoire Verdeaux na Ujumbe wake walipofika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Juni, 2023 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Picha ya pamoja na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Kimataifa ya Philip Morris, Gregoire Verdeaux na Ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Juni, 2023    

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AWAAPISHA VIONGOZI MBALIMBALI IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka kuwa Balozi kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Juni, 2023 . Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Eng. Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, TAMISEMI (Miundombinu) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Juni, 2023.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kamishna wa Polisi Benedict Michael Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Juni, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Iddi Seif Bakari kuwa Balozi nchini Uturuki kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 16 Juni, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan

KELELE NA MITETEMO INAUWA WATOTO NJITI 12,000 KWA MWAKA ULAYA PEKE YAKE

Image
Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kelele kuwa ni mojawapo ya kisababishi cha madhara katika maisha ya binadamu. Aidha, kwa mujibu wa “European Environmental Agency” (EEA, 2018) kelele zimeainishwa kuwa mojawapo ya visababishi vya vifo vya mapema vya watoto “Pre-mature death” ambapo takwimu zinaonyesha takribani watoto 12,000 hufariki kila Mwaka katika Bara la Ulaya”. Katika nchi yetu changamoto ya kelele zinazozidi viwango vilivyoainishwa na TBS zinatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia. Kwa siku za hivi karibuni, kelele zimeongezeka kwenye maeneo ya kazi na hivyo kusababisha matatizo ya kiafya ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza umakini katika mafunzo, ajali na kupungua uwezo wa kusikilizana. Vyanzo vikuu vya kelele hizi ni kumbi za starehe hasa biashara za vileo (baa), vyombo ya usafiri na usafirishaji (kama magari, ndege na treni), matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwan