DKT. SHEIN AFUNGUA TAWI LA BENKI YA CRDB CHAKE CHAKE, PEMBA Na Rajab Mkasaba, IKULU ZNZ RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein , ameeleza kuwa miongoni mwa changamoto zinazowakabili wateja wa Benki nyingi hapa nchini ni msongamano wa wateja pamoja na ucheleweshaji huduma na kuitaka Benki ya CRDB kuwa na mikakati katika kupambana na kadhia hiyo. Dk. Shein aliyasema hayo leo huko Chake Chake Pemba, katika sherehe ya ufunguzi wa Tawi jipya la Benki ya CRDB likiwa Tawi la 280 ndani ya mtandao wa benki hiyo kutoka matawi 19 iliyokuwa nayo mara tu baada ya kuanzishwa mnamo mwaka 1996. Katika hotuba yake, Dk. Shein alisema kuwa wananchi wanaeleza kwamba, miongoni mwa changamoto zinazosababisha msongamano ni kuwa benki za hapa nchini bado haziendani na kasi ya mabadiliko yanayotokea katika sekta ya fedha. Alieleza kuwa katika Siku ya Sherehe za Maadhimisho ya Mei Mosi, mwaka huu yaliyofanyika katika viwanja vya Mahonda, Unguja, Wafanyakazi...