Posts

Image
Dkt. Kigwangalla akabidhi gari la wagonjwa na vifaa vya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla mapema jana Mei 28.2017 amekabidhi gari maalum la kubebea wagonjwa (Ambulance) na vifaa vya Hospitali ikiwmo vitanda na Magodoro katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Mkoani Pwani. Dkt. Kigwangalla ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tukio hilo, mbali na kukabidhi gari hilo la wagonjwa na vifaa hivyo vya Hospitali kwa uongozi wa Hospitali na Wilaya akiwemo Mkuu wa Wilaya na Mbunge wa Jimbo hilo, aliweza kufanya ukaguzi wa ghafla kujionea mazingira ya Hospitali hiyo na kubaini mapungufu mbalimbali ambayoo ametoa maagizo kupatiwa ufumbuzi kabla ya kuchukuliwa hatua kwa uongozi wa Hospitali hiyo.   Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akikata utepe wakati wa kukaabidhi gari la wagonjwa hospitali ya Wilaya ya Mkuranga.   Mion...
Image
JICA YAPONGEZWA KWA KUDUMISHA USHIRIKIANO NA TANZANIA Na.Thobias Robert- MAELEZO. Serikali imelipongeza Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa ushirikiano wake na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika sekta za Kilimo Afya na Maendeleo ya Jamii kwa kutumia wataalam na uzoefu kutoka Japan. Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam leo na Mkurugenzi Msaidizi wa ushirikiano wa kiufundi kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw.Msafiri Marwa alipokuwa akiwaaga vijana wa kijapani waliokuwa wanajitolea katika sekta ya Kilimo na Maendeleo ya jamii hapa nchini. “Serikali ya Japan kupitia shirika lake la JICA imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na serikali ya Tanzania katika sekta mbalimbali kama vile kuwajengea uwezo Watanzania kupitia ufadhili wa masomo ya elimu ya juu nchini Japan na kuleta watu wa kujitolea katika miradi ya maendeleo hapa nchini,” alieleza Bw. Marwa. Aidha, Bw.Marwa ambaye alimuwak...
Image
DC MTATURU AWASIHI VIJANA KUDUMISHA NIDHAMU NA MSHIKAMANO Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Siasa Wilaya akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi ulioketi kuchagua uongozi wapya watakaoiongoza jumuiya hiyo. Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Ikungi wakimsikiliza mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo  Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kabla ya  kuchagua uongozi wapya kuongoza jumuiya hiyo ngazi ya Wilaya. Mbunge wa Jimbo La Singida Magharibi Mhe Elibariki Kingu  akizungumza na wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Um...

DK.SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI MBALI MBALI

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Dkt,Idris Muslim Hija kuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Joseph Abdalla Meza kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Bw.Juma Ali Juma kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar,kabla ya Uteuzi huo alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk....

JWTZ LAANZA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DKT MAGUFULI LA UJENZI WA UKUTA MERERANI-SIMANJIRO MKOANI MANYARA

Image
Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ laanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Meja Jenerali Michael Isamuyo atua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano. Helikopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuyo akitua Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kwa helkopta na kukagua maeneo ambayo ukuta utaanza kujengwa mara moja. Wachimba na wananchi wa Manyara wafurahi na waahidi ushirikiano. Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania JWTZ limenanza kutekeleza agizo la Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli.   Helkopta iliyombeba Meja Jenerali Michael Isamuhyo ikitua katika uwanja wa wazi wa Mererani, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara tayari kwa kukagua eneo litakalojengwa uzio kuzunguka kitalu A hadi D katika eneo la Madini la Tanzanite Mererani ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Pombe Ma...

KAMISHNA MKUU TRA AFANYA ZIARA YA KIKAZI TBL

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin (kulia) akimkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere wakati alipoongoza ujumbe wa Maofisa Waandamizi wa taasisi hiyo katika ziara ya kikazi katika kiwanda cha Bia cha Tanzania Breweries Limited, kilichopo Ilala jijini Dar e Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Group, Roberto Jarrin (aliyesimama) akielezea ujumbe wa Kamishna Mkuu wa TRA utendaji kazi wa kampuni hiyo. Meneja wa Afya na Usalama sehemuya kazi wa TBL Group, Renatus Nyanda (kushoto) akimweleza Kamishna Mkuu wa TRA (Kulia) na ujumbe wake utekelezaji wa kanuni za usalama wa kampuni kabla ya kuanza ziara ya kutembelea kiwanda ,wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa TBL,Roberto Jarrin. Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake wakipata maelezo ya mchakato wa kutengeneza bia kutoka kwa Meneja wa Kiwanda cha TBL cha Ilala-Calvin Martin. Mtaalam wa kuonja bia wa TBLGroup, Rebecca Semoka, (kushoto) akimweleza Kamishna Mkuu wa TRA na ujumbe wake m...