SERIKALI KUNUNUA NDEGE MBILI MPYA AINA YA JET
Baadhi ya Marubani wa
ndege mpya za Serikali aina ya Bombadier -8 Q400 zilizonunuliwa kutoka nchini
Canada wakifualtilia kwa makini hotuba mbalimbali za Viongozi wa Serikali
wakati wa hafla ya uzinduzi wa ndege hizo leo Jijini Dar es Salaam.
1
Rais Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali
mara baada ya uzinduzi wa ndege mpya za
abiria zilizonunuliwa na Serikali kutoka nchini Canada aina ya Bombadier- 8 Q400
leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ismail Ngayonga)
Na.
Sheila Simba
Dar
es Salaam
RAIS John Magufuli amesema Serikali imejipanga
kununua ndege mbili aina Jet zenye uwezo
wa kubeba abiria 160 na 242 pamoja na kutenga Tsh. Bilioni 100 kwa ajili ya ukarabati
viwanja vya ndege nchini.
Amesema hayo leo Jijini Dar Es
Salaam wakati wa uzinduzi wa ndege mpya mbili za abiria aina ya bombardier – 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali
kutoka nchini Canada ,na kuongeza kuwa ndege hizo zitasaidia kuboresha sekta ya
usafiri wa anga nchini.
“Ndege hizi ni nzuri sana,
kwani ukitaka kujenga nchi yenye uchumi wa kisasa huwezi kujenga bila kuwa na
ndege na ukitaka watalii lazima uwe na ndege” alisema Rais Magufuli
Alisema kuwa ndege hizo mbili zitakazonunuliwa na
Serikali zitakuwa na uwezo wa kubeba kusaidia watalii kuja nchini moja kwa moja
bila kutua nchi nyingine.
“Tunataka watalii wanaokuja
nchini kuja moja kwa moja bila kushuka nchi nyingine ili kuongeza mapato yetu
na kukuza utalii duniani na kuwa na ndege nyingi zaidi kama nchi nyingine” alisema
Rais Magufuli.
Akizungumzia ubora wa ndege za
bombardier alisema kuwa ndege hizo zinaenda na mazingira ya hapa nchini na zina
uwezo wa kutua katika viwanja vyenye lami na vile ambavyo havina lami na
uendeshaji wake ni wa gharama nafuu.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli
alisema kuwa ndege za bombardier zinatumia mafuta kidogo ikiwemo gharama ya tsh
Milioni 1 za mafuta kwa safari moja ikilinganisha na ndege nyingine zenye
kutumia tsh. Milioni 28 kwa safari.
Rais Magufuli aliitaka bodi ya
shirika la ndege Tanzania (ATCL) kufanya kazi nzuri ya kusimamia ndege hizo na
kutoa huduma nzuri na kuhakikisha wanapata faida ili serikali waweze kununua
ndege nyingi zaidi.
Alisema kuwa bodi ya ATCL wana
kazi kubwa ya kufanya kuboresha shirika hilo, kutokana na uzembe wa wafanyakazi
wake kutokuwa makini na kuwataka kupanga vizuri safari za ngede hizo kwani zina
uwezo wa kwenda mpaka nchi jirani.
“lazima mjue mnaingia kwenye
ushindani na washindani wenu hawawezi kufurahia wapo hujuma ili shirika
lisisonge mbele sasa fanyeni kazi”alisema Magufuli.
Aidha amewaomba ATCL kutotumia
mawakala katika kukatisha tiketi na kuzingatia muda wa safari ulipangwa na
kutoa huduma nzuri kwa wateja wao ili kukuza utalii nchini na kuwaomba watanzania kuwa wazalendo kwa
kutumia usafiri huo.
Kwa upande wake Waziri wa
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa alisema ndege hizo
zilizozinduliwa zinauwezo wa kubeba abiria 76 na abiria 6 wakiwa ni wa daraja
la biashara na 70 ni daraja la kawaida na ina uwezo wa kubeba mzigo wa tani
moja.
Ameongeza kuwa shirika la ATCL
lina upungufu mkubwa wa watalaamu katika maeneo mbalimbali ikiwemo, marubani,
wahandisi, wanasheria, maafisa biashara, wahasibu na menejimenti na hatua
inayosabisha shirika hilo kushindwa kujiendesha vizuri.
Waziri Mbarawa alisema kuwa ATCL
wamejipanga kutoa huduma za usafiri katika viwanja vya Dodoma, Dar Es Salaam
Bukoba, Tabora, Zanzibar, Mbeya, Kilimanjaro, Mtwara, Mwanza Kigoma, Arusha na
Comoro.
Comments
Post a Comment