BALOZI SEIF AKABIDHI MCHANGO WAKE ALOAHIDI KUCHANGIA UJENZI WA JENGO LA SITI BINT SAAD.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimkabidhi mchango wa shilingi Milioni 3,000,000/- Msaidizi Katibu wa Taasisi ya  Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar hapo Ofisini kwake ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.
 
Ahadi hiyo aliitoa wakati wa hafla maalum ya kuichangia Taasisi ya Kumbukumbu ya Siti Binti Saad iliyofanyika kwenye Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar miezi Miwili iliyopita ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.(Picha na – OMPR –ZNZ.)
 
Na. Othman Maulid. OMPR. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alisema Visiwa vya Zanzibar  vitaendelea kupata heshima Kimataifa kadri siku zinavyoaidi kuyoyoma katika Nyanja ya sanaa na utamaduni kufuatia kazi kubwa iliyokuwa ikifanywa  na Msanii mkongwe wa Visiwa hivi marehemu Sidi Binti Saad.
 
Alisema Mchango wa Siti Binti Saad enzi zake kupitia Taarab asilia umeweza kuleta faraja kwa wapenzi wa Muziki huo katika kudumisha Utamaduni wa Kiafrika ndani ya Mwambao wa Afrika Mashariki, Nchi za Ghuba pamoja na baadhi ya Mataifa ya Bara la Asia.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati wa kukabidhi mchango wa shilingi Milioni 3,000,000/- alizoahidi kutoa wakati wa hafla maalum ya kuichangia Taasisi ya Kumbukumbu ya Siti Binti Saad iliyofanyika kwenye Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar miezi Miwili iliyopita ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.
Alisema jitihada zilizochukuliwa na Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad ya katika azma ya kutaka kumuenzi Mwanamuziki huyo Nguli Afrika Mashairiki na Bara la Asia inafaa kuungwa mkono na wapenzi wote wa fani hiyo iwe ndani au nje ya Nchi.
Akipokea mchango huo wa Balozi Seif  Msaidizi Katibu wa Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar alimshukuru kiongozi huyo kwa kutekeleza ahadi aliyotoa kiasi kwamba imeleta faraja kwa Uongozi wa Taasisi hiyo.
Bwana Mohammed alisema katika kuthamini michango ya watoa ahadi  Taasisi hiyo imeamua kutoa cheti Maalum kwa wachangiaji hao ili iwe kumbu kumbu nzuri kwao na vizazi vyao kutokana na kuunga mkono jambo hilo muhimu.

Comments

Popular posts from this blog

LIGI KUU YA MUUNGANO YA NETIBOLI KATI YA POLISI MORO NA TTPL UWANJA WA GYMKHANA. TIMU YA POLISI MORO IMESHINDA 36-33

HAYA NDIYO BAADHI YA YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE