ALMASI YENYE THAMANI YA BILIONI 3.2 YAIPAISHA SEKTA YA MADINI TANZANIA
Tanzania imetajwa kuweka historia katika tasnia ya madini baada ya Almasi yenye Karati 512.15 kupatikana hivi karibuni katika eneo la Maganzo Mkoani Shinyanga na kuuzwa kwa jumla ya shilingi Bilioni 3.2.
Kuuzwa kwa jiwe hilo moja la almasi katika soko la madini mkoani Shinyanga ni muendelezo wa tija inayopatikana kupitia masoko hayo toka kuanzishwa kwake nchini,jumla ya shilingi bilioni 34.3 zimepatikana kwenye biashara ya dhahabu iliyofanyika katika kipindi cha mwezi mmoja tu kati ya Machi 17 mpaka Aprili 17 mwaka huu katika masoko ya madini kote nchini, kwa mujibu waziri wa Madini,Doto Biteko, aliyetoa taarifa hiyo hivi karibuni.



Comments
Post a Comment