
BOTI YA MIZIGO NA ABIRIA SITA YADAIWA KUPOTEA ZIWA TANGANYIKA,ILIKUWA IKITOKA KIGOMA KWENDA CONGO. Na Rhoda Ezekiel Kigoma. BOTI ya mizigo iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya Kalemi, imepotea katika ziwa Tanganyika ikiwa na Watu sita pamoja na Shehena ya vitungu gunia 110, ngano mifuko180 ,Mafuta ya taa dumu 20 na kreti za soda 70 ambayo mpaka sasa haijulikani ilipo. Akizungumza na Wanahabari Mkoani humo kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Fredinandi Mtui alisema Mnamo tarehe 23 januari majira ya saa 16:30 jioni boti iliyotengenezwa kwa mbao MV.Ngendo ya Buchuma, boti ya mizigo inayo milikiwa na Mussa Hamisi Mkazi wa ujiji Kigoma Manispaa ,iliondoka Katika Bandari ya Kibirizi ikiwa na shehena ya vitunguu, Ngano na watu sita kuelekea Congo ambayo mpaka sasa haijafika Congo na haijulikani ilipo. Mtui alisema mpaka sasa boti hiyo haijulikani ilipo na hakuna chochote kilicho onekana kati ya mizigo wala abiria Waliokuwa wam...