Posts

Showing posts from November, 2022

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UJENZI WA MABWAWA YA UMWAGILIAJI ITACHOCHEA KUKUA KWA SEKTA YA KILIMO

Image
  Naibu Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa An thony Mavunde amesema utekelezaji wa miradi ya mabwawa unaoendelea nchini hivi sasa utasaidia sana kukuza sekta ya kilimo nchini Tanzania na kuongeza eneo kubwa zaidi linalofanya kilimo cha umwagiliaji. Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 12 Novemba, 2022 wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa bwawa la Membe linalojengwa Wilayani Chamwino, Dodoma. "Katika bajeti ya mwaka 2022/2023 Serikali kupitia Tume ya Umwagiliaji imepanga kujenga jumla ya mabwawa 14 nchi nzima, likiwemo bwawa hili la Membe litakalo kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita Bilioni 12. Pamoja na bwawa hili kutumika katika shughuli za umwagiliaji, pia litawekwa miundombinu ya kusaidia unyweshaji maji mifugo, kupeleka maji ya matumizi ya majumbani kwa vijiji vinavyozunguka na kuwa sehemu ya utalii kwa wananchi mbalimbali, hatua ambayo itaongeza mapato ya Halmashauri ya Chamwino. Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ametuongezea bajeti Wizara ya Kilimo ambapo fedha nyingi zimee

WANAZUONI WA CHUO CHA DIPLOMASIA WAJADILI JUU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI INAVYOWEZA KUTUMIKA KATIKA UTEKELEZAJI WA DIPLOMASIA YA UCHUMI. TAREHE 8 NOVEMBA 2022

Image
Desderia Sabuni- Mkuu wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa Chuo cha Diplomasia akijadili juu ya Sensa ya watu na makazi (2022) inavyoweza kutumika katika Diplomasia ya Uchumi Tanzania.   Seif Ahmad Kushengo Mratibu wa Sensa Kitaifa akitoa maelezo ya awali juu ya Zoezi zima la Sensa livyofanyika kitaifa Balozi Mstaafu Modest Jonathan Mero akijadili Sensa ya Watu na Makazi inavyoweza kutumika katika Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. Tarehe 8 Novemba 2022 Desderia Sabuni mhadhiri  msaidizi na mkuu wa idara ya Uhusiano wa kimataifa na D iplomasia,mbobezi katika diplomasia ya uchumi  " Sensa inatoa dira ya uvutiaji wa wawekezaji,kiwango cha watu walioko nchini inaweza ikawa chachu ya fursa za uwekezaji nchini katika upatikanaji wa ajira,uwepo wa mitaji na uwepo wa soko." Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wakifuatilia mjadala wa Sensa ya Watu na Makazi inavyoweza kutumika katika Utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. Symphrosa Chaha Mratibu wa Mjadala wa Sensa ya Watu na Makazi inavy

WATAALAMU WA CHINA NA TANZANIA: ZIARA YA RAIS SAMIA NCHINI CHINA KUINUA UHUSIANO WA NCHI HIZI MBILI KWENYE NGAZI MPYA

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini China kuanzia kesho tarehe 2 hadi tarehe 4 mwezi Novemba, akiwa ni mkuu wa kwanza wa nchi ya Afrika kuizuru China baada ya Mkutano Mkuu wa 20 wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC). Kwenye semina ya kimataifa kuhusu ziara ya rais Samia nchini China na mustakbali wa uhusiano kati ya China na Tanzania iliyoandaliwa Oktoba 31 na Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, wataalamu na wasomi wa China na Tanzania wote wanaona kuwa ziara ya Rais Samia itainua uhusiano wa nchi hizo mbili kwenye ngazi mpya.  Akitaja matarajio yake kwa ushirikiano kati ya China na Tanzania, mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Prof. Liu Hongwu amesema pande hizo mbili zinapaswa kutilia maanani umuhimu wa kimkakati, kimsingi na kiuongozi wa ushirikiano kati ya China na Tanzania, na kuitumia vyema fursa inayotokana na ziara ya Rais Samia wa

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI BEIJING NCHINI CHINA KWA AJILI YA ZIARA YA KISERIKALI

Image
    Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Sam ia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Peking, Beijing nchini China kwa ajili ya ziara ya Kiserikali tarehe 02 Novemba, 2022

MIAKA MIWILI TANGU RAIS DK HUSSEIN ALI MWINYI ASHIKE HATAMU ZA KUIONGOZA...

Image