Posts

Showing posts from July, 2022

WIZARA YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA EXTENSIA YA UINGEREZA

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama  Connect To Connect,  tukio lililofanyika  Julai 25, 2022 jijini Dodoma. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama  Connect To Connect.  Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara hiyo, Bi. Lugano Rwetaka.  Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakati wa tukio la utiaji

MAKAMU WA RAIS MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA DORIS MOLLEL FOUNDATION JULAI 25

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akizungumza na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam tarehe 25 Julai 2022. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, mara baada ya Mazungumzo yaliofanyika Jijini  Dar es salaam  tarehe 25 Julai 2022. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango  tarehe 25 Julai 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation inayojihusisha na kusaidia Watoto wanaozaliwa kabla ya wakati (njiti) Bi. Doris William Mollel, Mazungumzo yaliofanyika Jijini Dar es salaam

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA USWISI NCHINI TANZANIA

Image
Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot akieleza jambo kwa  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani).   Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akimkaribisha Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot   tarehe 25 Julai, 2022 katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akiwa na   Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot pamoja na ujumbe wake  leo tarehe 25 Julai, 2022, mara baada ya kukutana naye katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Jijini Dar es salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akifafanua jambo kwa  Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe. Didier Chassot  tarehe 25 Jula, 2022, alipomtembelea katika ofisi ndogo za Ofisi hiyo Ji

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KWENYE SIKU YA MASHUJAA JIJINI DODOMA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki katika Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwa ajili ya Heshima ya Wimbo wa Taifa wakati ukipigwa kwenye Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka silaha za jadi (Ngao na Mkuki) kwenye mnara wa Mashujaa kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa iliyofanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi kwenye Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mashujaa Jijini Dodoma tarehe 25 Julai, 2022.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais Mhe.

WAKUU WA NCHI ZA EAC WASISITIZA UMUHIMU WA SOKO LA PAMOJA KATIKA KUKUZA UCHUMI WA KIKANDA

Image
  Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamesisitiza umuhimu wa soko la pamoja katika kukuza uchumi wakati waliposhiriki Mkutano Maalum wa Ngazi ya Juu wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mkutano huo maalum wa ngazi ya Wakuu wa Nchi uliofanyika tarehe 21 Julai 2022 na mkutano maalum wa ngazi ya Mawaziri uliofanyika tarehe 20 Julai 2022 jijini Arusha ni sehemu ya mikutano ya awali kuelekea Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika tarehe 22 Julai 2022. Katika mkutano huo Wakuu wa Nchi walijadili na kuyawekea msisitizo masuala mbalimbali ya hali ya halisi ya utekelezaji wa Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kuainisha changamoto zinazohitaji ufumbuzi wa pamoja katika kuyafikia malengo ya jumuiya hiyo. Akichangia mada wakati wa mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyeji wa mkutano huo, amesisitiza juu ya kukuza uzalishaji pamoja na