WAZIRI JAFO ATOA SIKU SABA KWA MTENDAJI MKUU WA SHIRIKA LA ELIMU KIBAHA KUANZA KUTEKELEZA UJENZI WA MRADI WA ULIOKUWA UMEKWAMA Naibu Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo akisalimiana kwa kumpa mkono mmoja wa wagonjwa mara alipofanya ziara yake ya kushtukiza katika hospitali ya tumbi kwaa ajili ya kuweza kufanya ukaguzi katika mradi wa upanuzi wa hospitali hiyo. PICHA NA VICTOR MASANGU NA VICTOR MASANGU, KIBAHA NAIBU Waziri wa Tamisemi Seleman Jafo amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa Tumbi na kutoa muda wa wiki moja kwa mtendaji mkuu wa Shirika la elimu Kibaha kuanza mara moja ujenzi kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa majengo baada ya kubaini umekwama kwa kipindi cha miaka saba bila ya kuendelezwa kitu chochote hali ambayo imesababisha kwa sasa eneo hilo kuota nyasi na kugeuka kuwa vichaka. Jafo akizungumza kwa masikitiko makubwa na baadhi ya watumishi wa hospitali ya Tumbi,pamoja na viongozi waandamizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa P...
Posts
Showing posts from September, 2017