
RAIS DKT MAGUFULI AMPOKEA MGENI WAKE RAIS RAMAPHOSA IKULU JIJINI DAR LEO. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa,mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwakaribisha wageni wao Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini Mh. Cyril Ramaphosa na mkewe Dkt. Dk Tshepo Motsepe, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo. Rais Ramaphosa amewasili hapa nchini jana jioni kwa Ziara ya Kitaifa ya siku 3 na baada ya hapo atahudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaofanyika Jijini Da...