WAZIRI JAFO AOMBA TAMASHA LA JAMAFEST KUKUZA KISWAHILI KWA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Selemani Jafo akizungumza alipotembelea katika Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalojulikana kama JAMAFEST linalofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania. Tamasha hilo limeanza Septemba 21 na linatarajiwa kuisha 28, 2019. Na Mwandishi Wetu. Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa Tamasha la utamaduni na sanaa la nchini za Afrika mashariki litumike kukiuza kiswahili ili na nchini mwanachama wa Afrika Mashariki waweze waongee lugha hii adhimu ambayo sasa ni lugha rasmi katika jumuiya za Afrika. Amesema hayo alipotembelea maonesho ya Tamasha la Uatamaduni na Sanaa la nchi za Afrika amashariki al-maalufu kama JAMAFEST linaloendelea kufanyika katika uwa nja wa Taifa jijini Dar es Salaam. "Nimetembelea mabanda mbalimbali na kujionea bi...