MFUKO WA PPF WAENDELEA KUKABIDHI VIFAA TIBA Mfuko wa Pensheni wa PPF umeendelea kukabidhi vifaa tiba katika hospitali na vituo vya afya nchini kulingana na sera yake ya uchangiaji na udhamini. Katika wilaya ya Kisarawe, Mfuko wa PPF umekabidhi vifaa tiba hivyo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI,Utumishi na Utawala bora Mhe. Selemani Jaffo kwa ajili ya hospitali ya Wilaya ya Kisarawe ambavyo ni vitanda 2 vya kujifungulia wakinamama, vitanda 4 vya wagonjwa wa kawaida, mashuka 56 na vifaa vinavyotumika kujifungulia wakinamama. Akipokea vifaa hivyo, Mhe. Jaffo alisema Mfuko wa PPF walichofanya ni jambo kubwa kwa vile hospitali za wilaya ya Kisarawe zilikuwa zikikabiliwa na changamoto katika sekta ya afya. Kwa upande wake, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele, alisema Mfuko umetoa vifaa tiba hivyo ikiwa ni muendelezo wa zoezi la kurudisha kwenye jamii kulingana na sera ya uchangiaji na udhamini ya PPF. Alisema Kisarawe ni wilaya ya nne kupa...
Posts
- Get link
- X
- Other Apps

BALOZI SEIF ALL IDD AVUTIWA NA UTENDAJI KAZI WA TASAF Picha ya juu na chini ,Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akizungumza na Wadau wa Maendeleo na viongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii-TASAF ofisini kwake mjini Unguja. Picha ya pamoja Balozi Seif Ali Idd akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF,Ladislaus Mwamanga baada ya kupata maelezo ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko huo kisiwani Zanzibar,anayewaangalia ni Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia ,Bwana Muderis Mohamed. Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Msingi Kizimbani,Unguja ambaye anatoka kwenye Kaya ya Mlengwa Wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini akikokotoa hesabu, anayemwangalia ni Msimamizi wa shughuli za TASAF katika Benki ya Dunia Bwana Muderis Mohamed. Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF ,Bwana Ladislaus Mwamanga(aliyesimama)akizungumza na baadhi ya wananfunzi wanaotoka katika Kaya za Walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika shule ya msingi Kiz...