MKUTANO WA SADC NGAZI ZA MAWAZIRI KUENDELEA KESHO

Mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unatarajiwa kuanza kufanyika jumanne ya Agosti 12,2019 ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi anatarajiwa kukabidhiwa Uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa ngazi za Mawaziri. Akizungumza wakati wa ukaguzi wa pikipiki mpya zinazotarajiwa kutumiwa katika mapokezi ya viongozi na wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa SADC unaoendelea Jijini Dar Es Salaam,waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi amesema serikali imekuwa ikiendelea na maandalizi mbalimbali ya mapokezi ya viongozi hao ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri ikiwemo magari na pikipiki achilia mbali hotel watakazofikia viongozi hao. Aidha Prof. Kabudi kwa niaba ya serikali,ameeleza kuridhishwa na kufurahishwa kwa namna vyombo vya habari Nchini vinavyoripoti kizalendo Mkutano unaoendelea wa Jumuiya ya Mae...