Posts

Kamati ya GFT yakagua maendeleo ya Mradi wa JNHPP, yaipongeza serikali

Image
Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) imeipongeza serikali kwa kupiga hatua zaidi katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo. Pongezi hizo zimetolewa na Meneja Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TAZARA) Mhandisi Fuad Abdallah kwa niaba ya wajumbe wote wa GFT wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo inayofanyika katika maeneo tofauti ya mradi huo, kuanzia June 6-11, mkoani Pwani.  Mhandisi Fuad alisema kuwa wamefanya ziara hiyo kwa kukagua maeneo mbalimbali ya mradi huo ambapo walikagua maendeleo ya ujenzi wa Tuta kuu la Bwawa, Kituo cha Kuchochea Umeme, Nyumba ya kuendeshea Mitambo ya kuzalisha umeme na Kingo za Bwawa (Saddle Dam) Muonekano wa eneo la kupeleka maji katika mitambo ya kufua umeme katika mradi wa JNHPP, Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT)walifa nya ziara ya kukaua eneo hilo...

DC IKUNGI AWATAKA WAKULIMA KUHIFADHI MAZAO YAO ILI WAYAUZE KWA BEI YENYE TIJA

Image
Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi na Wadau wa maendeleo wakiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro (kulia) wakivuta pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa ujenzi wa Ghala la Kisasa la kuhifadhi zao la Alizeti lililojengwa Kijiji cha  Mnang;ana, Kata ya Sepuka katika hafla iliyofanyika mwishoni mwa wiki wilayani humo mkoani Singida. Uzinduzi huo ukifanyika.Kutoka kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halashauri ya Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi. Mwenyekiti wa wilaya  hiyo, Ally Mwanga,kushoto ni Diwani wa Kata ya Sepuka, Halima Ng'imba na Mwakilishi wa Shirika la Wanawake na Jinsia la Umoja wa Mataifa (UN-WOMEN), ambaye pia ni Mtaalam wa Kitengo cha kuwawezesha wanawake kiuchumi,  Lilian Mwamdanga. Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika Wilaya ya Ikungi, Gurisha Msemo akiwa kwenye hafla hiyo. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, Ally Mwanga akizungumza kwenye hafla hiyo. Mwakilishi wa Shirika la Wanawake na Jinsia la Umoja wa Ma...

MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam aliporejea nchini akitokea Stockholm nchini Sweden alipohudhuria mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Stockholm +50.
Image
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (wa pili kulia) akisaini kitabu cha mahudhurio ya Wageni alipotembelea banda la maonesho la Wizara ya Mifugo na Uvuvi  yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma. Maonesho hayo yalikuwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake ni Juni 5, 2022. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mazingira, Sekta ya Uvuvi,  Bw. Melton Kalinga. Wengine kushoto ni Maafisa, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Sekta ya Uvuvi. Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki (kulia) akipatiwa maelezo kuhusu uandaaji na uhifadhi wa malisho ya mifugo na Afisa Mifugo Mkuu, Idara ya Utafiti, Mafunzo na Ugani (Sekta ya Mifugo), Bw. Deograsias Ruzangi alipotembelea banda la maonesho la Wizara ya Mifugo na Uvuvi  yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashuhudia utiaji Saini Mikataba ya miradi ya Maji kwa ajili ya Miji 28 katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi mbalimbali kabla ya kushuhudia utiaji Saini Mikataba ya miradi ya Maji kwa ajili ya Miji 28 kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 06 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishuhudia utiaji Saini Mikataba ya miradi ya Maji kwa ajili ya Miji 28 kwa Wakandarasi walioshinda zabuni kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 06 Juni, 2022. Viongozi mbalimbali, Wakandarasi walioshinda zabuni, pamoja na Wabunge wanufaika wa miradi ya Maji wakiwa katika viwanja vya Ikulu Chamwino kushuhudia utiaji Saini wa Mikataba ya miradi hiyo tarehe 06 Juni, 2022.    

CDF MABEYO KUSTAAFU MWEZI HUU, RAIS DKT. MWINYI AMPONGEZA

Image
Na Samir Salum, Lango la habari Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo kwa kutekeleza vyema majukumu yake katika kipindi chake chote cha utumishi ndani ya Jeshi hilo. Kupitia taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Juni 06, 2022 Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Charles Hilaly imeeleza kuwa Rais Dk. Mwinyi ametoa pongezi hizo wakati akizungumza na Jenerali Mabeyo ambaye alifika Ikulu Zanzibar kumuaga kufuatia kumaliza muda wa utumishi wake ndani ya Jeshi mwisho wa mwezi wa sita kwa mujibu wa sheria. Amesema kuwa Jenerali Mabeyo ni kiongozi ambaye alifanya kazi zake vema katika Jeshi hilo na alimpa ushirikiano mkubwa yeye na viongozi wenzake wakati  akiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa hatua ambayo ilimuwezesha kutekeleza mabadiliko mengi ndani ya Jeshi hilo. Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amemtakia kila la heri Jenerali Mabeyo katika maisha yake ya kustaafu hasa ikiku...

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIPOKEA TUZO YA BABACAR NDIAYE

Image
  Rais   @ SuluhuSamia   akipokea Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 kutoka kwa Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor kwa niaba ya Rais wa Benki hiyo Dkt. Akinumwi Adesina. Hafla ya Utoaji wa Tuzo hiyo imefanyika kwenye siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa AfDB, Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.