Posts

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO WA 22 WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC) JIJINI ARUSHA TAREHE 21 JULAI, 2022

Image
  FacebookShar Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza  na Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha AICC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 22 wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulionza tarehe 21 Julai, 2022 Jijini Arusha. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa nc...

MAKAMU WA RAIS AKIWASILI KATAVI KWA ZIARA YA KIKAZI

Image
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango leo tarahe 21 Julai 2022 akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Mpanda mkoani Katavi kwaajili ya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani humo.

MAADHIMISHO YA SIKU YA IDADI YA WATU DUNIANI KITAIFA YAFANA MANYARA

Image
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (wa pili kushoto), akiwasili katika viwanja vya shule ya Msingi Katesh B Wilayani Hanang’, mkoani Manyara, katika kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, wa pili kulia ni Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Makongoro Nyerere. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi itakayfanyika tarehe 23 Agostu, 2022 ili kupata takwimu sahihi za idadi ya watu ili kurahisisha mipango ya maendeleo, wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, Wilayani Hanang’, mkoani Manyara. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), Bw. Mark Bryan Schreiner, wakati wa kilele cha siku ya maadhimisho ya Idadi ya Watu Duniani, ikliyofanyika kitaifa Wilayani Hanang’, mkoani Manyara. Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. ...

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AMWAPISHA IGP WAMBURA TAREHE 20,JULAI 2022

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimvalisha Cheo kipya cha Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi (IGP) aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi  katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) Camillus Mwongoso Wambura kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi (IGP) katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbawe katika Hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 20 Julai, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimwapisha Balozi Luteni Jenerali Mathew Edward Mki...

MARUFUKU MICHANGO YA OVYO OVYO SHULENI

Image
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa nne kushoto) akivuta pazia kuashiria kuweka jiwe la msingi la mradi wa Kituo cha Afya cha Mtoa, kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Iramba Mkoani Singida wakati wa ziara yake ya kikazi wilayani humo leo. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Binilith Mahenge, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida Martha Gwau, Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk.Mwigulu Nchemba, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Alhajj Juma Killimbah,  Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Festo Dugange na Katibu Tawala Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko.

BUCKREEF YAKONGA MOYO WA WAZIRI BITEKO KWA KUTOA AJIRA KWA WAZAWA

Image
  WAZIRI wa Madini, Dkt. Doto Biteko ameupongeza mgodi wa dhahabu wa Buckreef kwa kutoa ajira kwa Watanzania wanaofanya kazi mbalimbali za uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huo. Dkt. Biteko amebainisha hayo Julai 16, 2022 wakati alipotembelea mgodi wa Buckreef mkoani Geita ili kujionea maendeleo ya shughuli za ujenzi na uchimbaji madini katika mgodi huo.  Amesema, mgodi wa Buckreef umetoa ajira za moja kwa moja 354 kwa Watanzania katika nafasi mbalimbali katika mgodi huo. Amesisitiza kwa wafanyakazi waliopewa ajira katika mgodi huo kuhakikisha wanajenga taswira nzuri kwa kuwa wazalendo na waaminifu katika kazi zao.  Amesema, kupitia uaminifu wawekezaji watatoa fursa zaidi kwa Watanzania kuweza kufanya kazi mbalimbali. Aidha, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa, miradi yote iliyopo kwenye Sekta ya Madini itaendelezwa ili watanzania wanufaike na rasilimali madini na kuongeza Pato la Taifa.  "Matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kw...

MAKATIBU WAKUU WA SADC WAANZA MAANDALIZI YA MKUTANO WA 24 WA KAMATI YA MAWAZIRI

Image
Mkutano wa 24 wa Kawaida wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Ushirikiano katika masuala ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (MCO) utafanyika jijini Pretoria, Afrika Kusini kuanzia tarehe 16 hadi 19 Julai, 2022.    Mkutano huo umetanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu unaofanyika tarehe 16 na 17 Julai 2022 ambapo ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kamati hii unaongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab ambaye anamwakilisha Katibu Mkuu, Balozi Joseph Sokoine.    Mkutano wa 24 unalenga pamoja na mambo mengine k upokea na kujadili agenda mbalimbali zikiwemo m apitio ya utekelezaji wa maamuzi ya Mkutano wa 23 wa MCO na Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC; Hali ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya kanda; na tathmini ya hali ya Ulinzi na Usalama katika Kanda pamoja na Tathmini ya athari zitokanazo na mgogoro unaoendelea katika bara la Ulaya.   Viongozi wengine ku...