
BALOZI SEIF AKABIDHI MCHANGO WAKE ALOAHIDI KUCHANGIA UJENZI WA JENGO LA SITI BINT SAAD. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimkabidhi mchango wa shilingi Milioni 3,000,000/- Msaidizi Katibu wa Taasisi ya Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar hapo Ofisini kwake ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar. Ahadi hiyo aliitoa wakati wa hafla maalum ya kuichangia Taasisi ya Kumbukumbu ya Siti Binti Saad iliyofanyika kwenye Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar miezi Miwili iliyopita ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.( Picha na – OMPR –ZNZ.) Na. Othman Maulid. OMPR. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Visiwa vya Zanzibar vitaendelea kupata heshima Kimataifa kadri siku zinavyoaidi kuyoyoma katika Nyanja ya sanaa na utamaduni kufuatia kazi kubwa iliyokuwa...