MAKALA: WIKI YA SHERIA NA SIKU YA SHERIA NCHINI, 2017
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikagua gwaride maalum lililoandaliwa, ukaguzi wa gwaride hili huashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama kwa mwaka husika. Na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania Nchi yoyote yenye kuzingatia misingi ya Utawala wa Sheria, huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta amani na Maendeleo ya kiuchumi katika taifa husika. Hii inajidhihirisha kupitia Kaulimbiu ya Wiki ya Sheria na Siku ya Sheria nchini, 2017 ambayo ni ‘Umuhimu wa Utoaji Haki kwa wakati kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.’ Kauli mbiu hii ina maana ya kuwa kukamilishwa mapema kwa mashauri ya jinai, Rushwa na Uhujumu Uchumi ambayo yanaendeleza amani na usalama katika jamii ni chachu ya maendeleo ya uchumi. Hivi karibuni Mahakama ya Tanzania iliadhimisha Siku ya Sheria nchini, ambayo huashiria kuanza rasmi kwa mwaka wa Mahakama ambapo shughuli za usikilizaji wa Mashauri huanza rasmi. Kwa mwaka huu, sherehe za Siku ya Sheria nchini ziliadhimishwa rasmi tarehe 02.02.20...