Mawaziri wa Zanzibar watembelea Wizara ya Ardhi ya SMT kwa ajili ya kubadilishana uzoefu

Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwaelezea
Mawaziri kutoka Zanzibar jinsi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kinavyorahisisha kutoa Huduma za
Ardhi bila usumbufu kwa Wananchi. Kuanzia
Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.
Mohamed Aboud, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar
Mhe. Hamad Rashid, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar
Mhe. Salama Talib na Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu
Kayandabila.

Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akimuonesha
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed
Aboud jinsi ya kutumia mashine ya kutolea huduma za Ardhi katika kituo
cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri
wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib akipata
maelezo kutoka kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe
William Lukuvi jinsi Wizara yake ilivyofanikiwa kuyapatia ufumbuzi
masuala mbalimbali ya Ardhi na kuwaondolea usumbufu Wananchi katika
kupata huduma za Ardhi. Kushoto ni Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt.
Yamungu Kayandabila.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwa na
ujumbe wa Mawaziri kutoka Zanzibar walipofika ofisini kwake.
Wananchi
wakipata Huduma za Ardhi katika Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Comments
Post a Comment