MAKAMU WA RAIS APONGEZA KIWANDA CHA IVORY FOOD& BEVARAGE IRINGA

Makamu wa  Rais  Samia  Suluhu  Hassan  akitembelea  kiwanda  cha Ivori Food & Bevarage leo 

Makamu  wa  Rais  Samia  Suluhu Hassan  katikati  akiongozana na  mkuu wa  mkoa wa Iringa Amina Masenza kushoto na mkurugenzi wa  kiwanda  cha Ivori Food & Bevaragena mkurugenzi Mtendaji Suhail Esmail Thakore



Mkuu  wa   mkoa wa Iringa  Amina Masenza akisalimiana  makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan  leo 
mkurugenzi Mtendaji wa  kiwanda   cha  Ivory Bw Suhail Esmail Thakore akitoa  taarifa ya  kiwanda  hicho 


 Makamu  wa  Rais  Samia Suluhu  Hassan  akizungumza  baada ya  kutembelea  kiwanda  cha Ivory  Iringa 

Na  Matukiodaima Blog 


MAKAMU
wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
TanzaniaSamia Suluhu Hassan  amepongeza
uwekezaji  mkubwa  uliofanywa na kiwanda cha Ivori Food &
Bevarage cha Iringa kuwa  ni  hatua
kubwa  ya  mapinduzi
ya  serikali ya viwanda  nchini .

Akizungumza 
leo  baada ya  kutembelea 
kiwanda   hicho  eneo la
Ipogolo makamu  wa  Rais
alisema  kuwa   serikali imejikita  kuweka
mazingira  bora kwa  wawekezaji
pamoja  na  kuona
wananchi  wanapata  ajira
katika  viwanda   hivyo .


Ndugu  zangu  tunaelekea
kwenye  Tanzania  ya
viwanda  kwa  kujenga
uchumi  mpya  katika
nchi   yetu kama  tukiwa na
viwanda vitano ama  kumi kama   hivi
basi  uchumi  wetu
utazidi  kukuwa  zaidi “

Hata 
hivyo alitaka  ili  kuwa na uchumi  zaidi na
viwanda  kuweza  kusonga mbele
ni  vema  kila mwananchi  kutunza amani
na  kuepuka  kuvuruga amani iliyopo .

Ninachowaomba  ndugu  zangu
tuchape kazi  Tanzania  yetu
isonge  mbele  hivyo
wote  ambao  mmepata
kazi katika  kiwanda   hiki
chapeni kazi  ili  nchi 
yetu   izidi  kuendelea
kiuchumi “

Alisema 
kuwa  kiwanda  hicho
kimekuwa  nguzo  kubwa ya
uchumi  katika  mkoa
wa  Iringa na  Tanzania
kwani  ni  miongoni mwa
viwanda  ambavyo  vinafanya 
vizuri  na  vinazidi
kujitanua  zaidi kwa  kufunga
mashine  mpya  za
kisasa .

Akitoa
taarifa  ya  kiwanda
hicho  cha Ivori Food &
Bevarage na mkurugenzi Mtendaji Suhail Esmail
Thakore  alisema  kuwa
kiwanda  kilianzishwa  mwaka 2007
na  kuwa  kiwanda 
hicho  kinajishughulisha  na
uzalishaji  mbali mbali  zikiwemo
pipi ,Cocoa Poda, Tomato
Sauce  na  Chocolate .

  Kuwa
kiwqanda   hicho  wakati
kinaanzishwa  kilikuwa na  wafanyakazi 20  na
kilianza  na mtaji  wa
fedha  kiasi cha  shilingi milioni 70   kikiwa
kinazalisha  Tomato Sauce .
  Upanuzi
wa  kiwanda    ulianza mwaka  2009
tulifanya  upanuzi  wa
kiwanda   kwa  kuanzisha
uzalishaji wa  pipi  Ivory
kwa  mtaji  wa
shilingi  bilioni 1.5 mwaka  2014
tulianzisha   kiwanda cha  Chocolate
na  cocoa  Poda kwa mtaji  wa
shilingi  bilioni 3”
 Alisema
kuwa  kiwanda   kinatumia
malighafi   toka  ndani
ya  nchi  ikiwemo cocoa
tpoka  Kyela ,nyanya  toka
Ilula wilaya ya  Kilolo  na mahindi
toka  Iringa  , Ruvuma
na  Rukwa .

Hata   hivyo
alisema  kutokana na  uzalishaji
mzuri  na ubora  wa
bidhaa za   kiwanda  hicho wamefanikiwa  kushindana
na  masoko  ya
nje  kama  Kenya na
nchi  nyingine  hasa
katika  soko la  Pipi na
cocoa Poda .
Tulipo  anzisha
kiwanda  cha  pipi
tulikuwa na  viwanda  saba 
katika  soko la Tanzania  hadi 
sasa   viwanda    vilivyobaki
ni  viwili  na
tuna  mshindani   aliyebaki
ambaye  ana hali  mbaya
zaidi  tunaweza  kupata
masoko  katika  nchi
za Kenya ,  Uganda , Msumbiji ,
Burundi  na  Jamhuri
ya  kidemokrasia  ya
congo “
Alisema  kuwa 
kiwanda  kimeweza  kutoa
ajira  kwa  vijana
150  kati ya  hao
ajira  ya  kudumu
ni  watu  105
na  ajira ya  muda
n  watu  45 .
Pia  alisema 
kiwanda   hicho  kimeweza kuzaa kiwanda  kingine 
cha pipi  ambapo ujenzi   umekamilika
na  mashine   zimeshafika
ndani ya  kipindi  cha miezi mitatu  hadi  mine
 kitaanza kazi  ya uzalishaji
na  kutoa ajira kwa  vijana 60.
Bwana  Thakore alizitaja  changamoto
zinazokabili  kiwanda  hicho
kuwa  ni sukari  ya
viwandani ambayo  waliomba tani
3000  kwa mwaka huu  wa serikali 2017/18  ila
wamepata  tani 416  mwezi
Oktoba .
  Jumla ya
mzigo  wote  ambao
tumepata  ni tani 848 ambao  tumepokea
lakini baada ta  timu  ya
Vwrification  kupita  kwetu
na  tarehe  19
Januari  mwaka  huu
hadi  sasa  hakuna
majibu  yoyote  juu ya
vibali  vingine  kwa bodi ya
sukari  wamekataa  kutoa
vibali   vingine  hadi pale
ambapo  maelekezo  yatatolewa 
hivyo  basi  tunakosa
mwelekeo  wa  huko mbele
kwa kuwa malighafi  hiyo  muhimu  
ikiadimika  tutalazimika  kusimama
uzalishaji “
Alisema  wanaomba serikali  kusikia
kilio  chao  kwa
kutafuta  ufumbuzi wa  haraka wa
jambo hilo zito .

“ Ili   serikali
itusaidie   kuhakikisha  bodi ya
sukari  iweze   kutupa
muongozo  wa  juu ya
vibali  vingine  kabla
hatujaagiza mzigo mwingine
na  kabla ya akiba  tuliyo nayo
kuisha  kwa maana  mzigo
hadi ufike kiwandani   unachukua  muda wa miezi miwili  jambo
hili  ni muhimu  sana
katika maendeleo ya  viwanda  vyetu
na kwa  kuwa  tunaongeza mitambo  ya pipi 
tunahitaji  Sukari kwa  wingi
kutokana na kuongezeka  uzalishaji

Alisema  baada ya
serikali ya a wamu ya  tano chini
ya Rais Dkt  John  Magufuli 
kuingia madakani  soko la
ndani  limeongezeka   kutokana na
serikali   kubana njia  za  kukwepa
ushuru  wa bandarini .

  Kubanwa
kwa  mianya ya  ukwepaji kodi
kumesaidia   sana  kuongeza
soko la  bidhaa  zetu
awali  bidhaa  kutoka
nje  zilikuwa zikiuzwa kwa  bei
ndogo hasa  baada ya  ukwepaji
wa kodi   na  kuhatarisha
bidhaa  za ndani .

Comments

Popular posts from this blog

HAYA NDIYO BAADHI YA YALIYOSABABISHA UCHAGUZI ZANZIBAR UFUTWE

LIGI KUU YA MUUNGANO YA NETIBOLI KATI YA POLISI MORO NA TTPL UWANJA WA GYMKHANA. TIMU YA POLISI MORO IMESHINDA 36-33