KASI YA SERIKALI YA JPM KWENYE KOROSHO; SASA VIWANDA VYAAMKA.
Korosho ikiwa tayari kwa kusafirisha Tanzania ni mmoja wa wazalishaji wakuu zaidi wa korosho katika Afrika, mauzo ya karosho ya Tanzania huchangia asilimia kumi na tano ya fedha za kigeni. Tanzania ni mkulima wa 8 mkubwa zaidi duniani na wa 4 katika Afrika. Takwimu iliyotolewa mwaka 2012 na Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Tanznaia imekuwa imefanya vizuri katika uzalishaji wa zao la korosho tangu kabla ya uhuru, hata hivyo, udhibiti mbaya na ukosefu wa malipo ya kuaminika kwa wakulima wamesababisha uzalishaji wa korosho kutokuongezeka. Kwa kawaida mmea hupandwa katika mikoa ya kusini ya pwani, Mtwara, Kilwa na Dar-es-Salaam. Uuzaji wa korosho huendeshwa na Bodi ya Korosho ya Tanzania, kwa njia ya ushirika mbalimbali wa wakulima. Zaidi ya asilimia tisini ya mauzo ya nje ni nchini India, Ukosefu wa makampuni ya ubanguaji wa wa korosho ha Tanzania, umezipa faida kubwa nchi za kigeni kwa kuzalisha maelfu ya kazi kupitia korosho zinazotoka Tanzania. Serik...