KELELE NA MITETEMO INAUWA WATOTO NJITI 12,000 KWA MWAKA ULAYA PEKE YAKE

Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kelele kuwa ni mojawapo ya kisababishi cha madhara katika maisha ya binadamu. Aidha, kwa mujibu wa “European Environmental Agency” (EEA, 2018) kelele zimeainishwa kuwa mojawapo ya visababishi vya vifo vya mapema vya watoto “Pre-mature death” ambapo takwimu zinaonyesha takribani watoto 12,000 hufariki kila Mwaka katika Bara la Ulaya”. Katika nchi yetu changamoto ya kelele zinazozidi viwango vilivyoainishwa na TBS zinatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia. Kwa siku za hivi karibuni, kelele zimeongezeka kwenye maeneo ya kazi na hivyo kusababisha matatizo ya kiafya ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza umakini katika mafunzo, ajali na kupungua uwezo wa kusikilizana. Vyanzo vikuu vya kelele hizi ni kumbi za starehe hasa biashara za vileo (baa), vyombo ya usafiri na usafirishaji (kama magari, ndege na treni), matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwan...