KELELE NA MITETEMO INAUWA WATOTO NJITI 12,000 KWA MWAKA ULAYA PEKE YAKE

Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kelele kuwa ni mojawapo ya

kisababishi cha madhara katika maisha ya binadamu. Aidha, kwa mujibu

wa “European Environmental Agency” (EEA, 2018) kelele zimeainishwa kuwa

mojawapo ya visababishi vya vifo vya mapema vya watoto “Pre-mature death”

ambapo takwimu zinaonyesha takribani watoto 12,000 hufariki kila Mwaka

katika Bara la Ulaya”.

Katika nchi yetu changamoto ya kelele zinazozidi viwango vilivyoainishwa

na TBS zinatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo

matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia. Kwa siku za hivi karibuni, kelele

zimeongezeka kwenye maeneo ya kazi na hivyo kusababisha matatizo ya

kiafya ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza

umakini katika mafunzo, ajali na kupungua uwezo wa kusikilizana.


Vyanzo vikuu vya kelele hizi ni kumbi za starehe hasa biashara za vileo (baa),

vyombo ya usafiri na usafirishaji (kama magari, ndege na treni), matumizi

ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwanda vikubwa na vidogo

(Karakana za kuchomelea, ufyatuaji matofali, mashine za kusaga na kukoboa

nafaka), majenereta, matangazo ya biashara mitaani, shughuli za ujenzi, nyumba za ibada n.k.



SHERIA NA SERA ZINAZOONGOZA UDHIBITI WA

KELELE NA MITETEMO

Udhibiti wa kelele na mitetemo nchini unasimamiwa na Sheria mbalimbali

zikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 pamoja na

Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa Kelele na Mitetemo) za

Mwaka 2015; Sheria ya Usalama Kazini ya Mwaka 2003; Sheria ya Afya ya

Jamii ya Mwaka 2009; Sheria ya Jumuiya [Sura ya 337 Marejeo ya 2002];

Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa [Sura 204 Marejeo ya 2002] na Kanuni za

Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018; Sheria ya Ardhi [sura 113 Marejeo ya

Mwaka 2019] na Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 pamoja na Kanuni

zake za Mwaka 2018.

Sheria na Kanuni hizi zimeelekeza shughuli zote zenye madhara zifanyike

mbali na makazi ya watu na hivyo shughuli zenye kelele kufanyika mbali na

makazi ya watu ili kupunguza madhara kwa afya ya binadamu na mazingira.




BARAZA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA (NEMC)

Katika kuhakikisha kelele na mitetemo zitokanazo na shughuli mbalimbali

zinadhibitiwa, Baraza litafanya yafuatayo:

a. Kuendelea na ukaguzi wa maeneo ya biashara na kutoa

maelekezo mbalimbali ikiwemo Amri na Ilani za kudhibiti kelele.

b. Kuanisha na kutangaza maeneo ambayo kelele haziruhusiwi

(Noise Control Zone).

c. Kusimamia uanishaji wa ramani za maeneo yenye kelele

zilizopitiliza na kuandaa Mkakati wa udhibiti.

Mwongozo wa Kitaifa wa Udhibiti Kelele na Mitetemo

d. Kufanya tafiti za mara kwa mara kubaini hali ya uchafuzi wa

mazingira utokanao na kelele na mitetemo.

e. Kutoa elimu kwa jamii na maafisa mazingira kuhusu majukumu

yao katika udhibiti wa kelele na mitetemo.

f. Kupokea taarifa za malalamiko yanayohusu kelele na mitetemo.




Comments

Popular posts from this blog

JUHUDI ZA MWALIMU NYERERE KATIKA KUKUZA NA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII NCHINI