Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) imetoa miezi sita kwa Taasisi na Mashirika yote kulipa madeni ya ankara wanayodaiwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na endapo watashindwa kufanya hivyo watakatiwa huduma hiyo

Agizo hilo limetolewa mkoani Mbeya na Mwenyekiti wa Kamati ya PAC , Livingtone Lusinde wakiwa katika ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika kutekeleza Miradi ya Umeme Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati wa Vijijini( REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme nchini Tanesco. Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Rungwe, Chalya Julius (katikati), Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Livingstone Lusinde (kulia) wakati wa ziara ya kukagua matumizi ya fedha za Serikali katika Miradi ya umeme vijijini wilayani humo, mkoani Mbeya. Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), wakielezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) namna ambavyo kifaa maalum kinachofahamika kama umeme tayari (UMETA) umeme tayari kinavyofanya ...