Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali ( PAC) imetoa miezi sita kwa Taasisi na Mashirika yote kulipa madeni ya ankara wanayodaiwa na Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na endapo watashindwa kufanya hivyo watakatiwa huduma hiyo
Agizo hilo limetolewa mkoani Mbeya na Mwenyekiti wa Kamati
ya PAC , Livingtone Lusinde wakiwa katika ziara ya Wajumbe wa Kamati hiyo wakikagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika kutekeleza Miradi ya Umeme
Vijijini inayotekelezwa na Wakala wa Nishati wa Vijijini( REA) kwa kushirikiana
na Shirika la Umeme nchini Tanesco.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya Rungwe, Chalya Julius (katikati), Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Livingstone Lusinde (kulia) wakati wa ziara ya kukagua matumizi ya fedha za Serikali katika Miradi
ya umeme vijijini wilayani humo, mkoani
Mbeya.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali (PAC), wakielezwa na Naibu Waziri
wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani (katikati) namna ambavyo kifaa maalum
kinachofahamika kama umeme tayari (UMETA) umeme tayari kinavyofanya kazi
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa (katikati) akiwa na Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC), pamoja na Naibu Waziri wa
Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, walipomtembelea ofisini kwake, wakati
wa ziara ya kukagua matumizi halisi ya fedha za Serikali katika utekelezaji wa
Miradi ya Umeme Vijijini.
Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini wakiwa katika kikao
na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali,kutoka kulia ni Afisa
wa Bunge wa Wizara ya Nishati na Madini,
Kalori Mmasy, Meneja wa Tanesco Kanda ya Nyanda za juu kusini, Mhandisi
Salome Mkomolwa na Mhandisi Edson Ngabo.
Comments
Post a Comment