Posts

JE UNAJUA ZANZIBAR ILIBEBA JUKUMU LA SAFARI YA APOLLO 11 20.7.1969, ...

Image
ZANZIBAR, KIMYA  KIMYA  ILICHUKUA JUKUMU MUHIMU KATIKA SAFARI ZA ANGA   Z A MAREKANI KUTUA  MWEZI NI.THAMANI YA NCHI YETU ISIYOSEMWA MARANYINGI Vituo  viwili  vya satelaiti barani Afrika vilikuwa viunganishi muhimu vya safari hizi za  anga za juu  za  wamarekani .   Mnamo Julai 20, 1969,  Apollo  11 iliweka historia ya ulimwengu ilipotua kwenye mwezi. Lakini hadi leo, watu wachache wanajua kuhusu vituo vya anga vya Kano, kaskazini mwa Nigeria, na Tunguu, Zanzibar, ambavyo vilisaidia kuweka msingi ambao hatimaye ulifanikisha misheni ya  Apollo  11.   Vita Baridi kati ya Muungano wa Kisovieti na Marekani vilijitokeza kwa kasi katika mbio kubwa ya anga za juu. Kabla ya kutua kwa mwezi kwa mafanikio kutokea, M arekani  ilihitaji kujaribu vyombo vya anga vya juu na visivyo na rubani. Mnamo Oktoba 1958, Utawala wa Kitaifa wa Anga na Anga (NASA) ulizindua Mradi wa  Mercury , mradi wa miaka mitano, wa dola mili...

KWA NINI MAWAZIRI WANAMAAFISA WAO WA HABARI? VITENGO VYA HABARI KILA TAA...

Image

MAKAMU WA RAIS UFUNGUZI WA MWAKA WA MAHAKAMA YA AFRIKA - ARUSHA

Image
Mpango akizungumza na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Imani Aboud wakati alipowasili Makao Makuu ya Mahakama hiyo mkoani Arusha kuhudhuria ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu   tarehe 20 Februari 2023. (Kulia ni Makamu wa Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu Jaji Blaise Tchikaya) Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akihutubia Majaji, Viongozi na Watumishi mbalimbali wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na watu wakati wa Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama hiyo uliofanyika Makao Makuu ya Mahakama hiyo mkoani Arusha  tarehe 20 Februari 2023 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akipokea Vitabu vya Hukumu mbalimbali zilizotolewa na Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu tangu kuanzishwa kwakwe kutoka kwa Rais wa Mahakama hiyo Jaji Imani Aboud mara baada ya  Ufunguzi wa Mwaka wa Mahakama ya Afrika ya Ha...

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI WA LONGPING YA CHINA

Image
 

VODACOM Yaanzisha Huduma Mpya Kwa Walemavu Wasiosikia

Image
Mkurugenzi wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni Kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Dar es salaam Habibu Mrope, akifuatilia uzinduzi wa huduma ya alama ya vidole kwa wa wateja wenye changamoto ya kusikia leo Februari 15, 2023. Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Vodacom, Herieth Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kuzindua huduma mpya ya matumizi ya alama ya kwa wateja wao ambao wana changamoto ya kusikia. Baadhi ya walemavu wasiosikia wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Vodacom.   Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania imeanzisha huduma itakayowawezesha watu wenye ulemavu wa kusikia kuweza kupata huduma ya kuwasiliana na wahudumu wa mtandao huo kwa njia ya alama za vidole. Imesema imeazisha huduma hiyo kwa viziwi ili kuhakikisha kila mteja wao anapata huduma anayostahili bila kuachwa nyuma kwasababu ya kuwa na changamoto ya kusikia lakini pia ili waweze kuwasiliana. Hayo y...

RAIS DKT SAMIA AANDIKA HISTORIA AFANYA UWEKEZAJI MKUBWA WA ZAIDI YA BILIONI 2 KITENGO CHA MIONZI HOSPITALI MKOA WA TANGA

Image
  Mkuu wa Idara ya Kitengo cha Mionzi na Picha katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo,Dkt Goodluck Mbwilo akizungumza kuhusu uwekezaji huo mkubwa uliofanywa na Rais Dkt Samia Suluhu kwa ajili ya ujenzi wa jengo na ununuzi wa Mashine ya CT scan ambao umesaidia kwa asilimia kubwa kuwapunguzia mzigo wananchi waliokuwa wakifuata huduma hiyo mikoa mengine, kulia ni Mteknolojia Mionzi katika Hospitali hiyo, Bw. Athumani Rajabu Mashine ya CT Scan inayotumika katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga- Bombo Mteknolojia Mionzi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo  Bw. Athumani Rajabu akizungumza wakati  akionyesha mashine kubwa waliyoipata yenye uwezo mkubwa wa kufanya uchunguzi kwa wagonjwa zaidi ya 100 kwa siku na Serikali imefanya kama zawadi kwa wananchi wa  mkoa wa Tanga. Mteknolojia Mionzi katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo Bw.  Athumani Rajabu, akifanya matayarisho ya awali kabla ya kuwahudumia wagonjwa wanaohitaji kipimo cha CT Scan Na Oscar As...

RAIS SAMIA AWAAPISHA VIONGOZI IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) akiwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo (Mb) Balozi Mhe. Pindi Hazara Chana, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Said Othman Yakub wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, 15 Februari, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 15 Februari, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi Mhe. Pindi Hazara Chana (Mb) kuwa Waziri wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es salaam tarehe 15 Februari, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Said Othman Yakub kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo katika hafla iliyofanyika ...