VODACOM Yaanzisha Huduma Mpya Kwa Walemavu Wasiosikia


Mkurugenzi wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni Kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Dar es salaam Habibu Mrope, akifuatilia uzinduzi wa huduma ya alama ya vidole kwa wa wateja wenye changamoto ya kusikia leo Februari 15, 2023.

Mkurugenzi wa huduma kwa wateja Vodacom, Herieth Lwakatare akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) baada ya kuzindua huduma mpya ya matumizi ya alama ya kwa wateja wao ambao wana changamoto ya kusikia.

Baadhi ya walemavu wasiosikia wakiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya simu ya Vodacom.

 Kampuni ya simu za mkononi Vodacom Tanzania imeanzisha huduma itakayowawezesha watu wenye ulemavu wa kusikia kuweza kupata huduma ya kuwasiliana na wahudumu wa mtandao huo kwa njia ya alama za vidole.

Imesema imeazisha huduma hiyo kwa viziwi ili kuhakikisha kila mteja wao anapata huduma anayostahili bila kuachwa nyuma kwasababu ya kuwa na changamoto ya kusikia lakini pia ili waweze kuwasiliana.

Hayo yameelezwa leo na Mkurugezi wa huduma kwa wateja wa Vodacom, Herieth Lwakatare Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo iliyouzuliwa na chama cha viziwi Tanzania (CHAVITA).

Lwakatare amesema, wamekuwa wakipata wateja wa aina mbali mbali ambao wanachangamoto na mahitaji tofauti tofauti hususani wenye changamoto ya kiafya kufuatia hali hiyo wakanaona ni vema kuja na huduma hiyo kwa walemavu wa viungo na wameanza na viziwi.

"Ili kuhakikisha huduma hiyo inafika nchi nzima, mpaka sasa tumetoa mafunzo kwa wafanyakazi na watoa huduma watu 30 ili waweze kuwasiliana kwa njia ya wasap (video call) na mteja ambaye ni kiziwi ili aweze kupata msaada kama wateja wengine," Amesema.

Amesema huduma hiyo pia inatolewa katika maduka ya Vodacom na kwa wateja ambao hawezi kufika kwenye maduka hayo basi wanaweza kupiga simu kupitia wasap (video call) na kuwasiliana na muhuduma ambaye atawahudumia kwa lugha ya alama ya vidole.

"Katika maduka yetu hapa Dar es Salaam tumeweza kuweka watafsiri wa alama za vidole waweze kuongea na wateja ambao ni viziwi hivyo mteja anaweza kutemebelea maduka yetu kadhaa," amesema.

Amesema huduma hiyo wanayoitoa siyo kwa viziwi tu bali pia tumetengeneza njia ambayo inamuwezesha mteja anayetumia kiti cha magurudumu (Wheelchair) aweze kupita kwa urahisi na kupata huduma.

Pia amesema wanaangalia ubunifu wa kutumia njia ya sauti ili kuweza kuwasaidia wenye changamoto ya kuona kuweza kutumia sauti yake kama njia ya kujitambulisha ili aweze kutumia M-pesa na kama amesahau namba yake ya siri basi anaweza kuirudisha kwa kutumia sauti yake.

Aidha alisema lengo Kuu la kuwa pamoja na chavita ni kusikiliza wateja wao na kupata maoni zaidi ili kuweza kuboresha humuda hii ya alama za vidole.

Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Kituo cha Sanaa na Utamaduni Kwa Viziwi Tanzania (KISUVITA) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Dar es salaam Habibu Mrope ameishukuru kampuni ya Vodacom kwa kubuni huduma ya lugha la alama ambayo sasa imemuwezesha mawasiliano yao kuwa na rahisi hapa nchini.

"Binafsi nimefurahi sana, kama mlivyoona viziwi wamejaa na wamefurahi mazingira ya huduma ni rafiki na salama kwetu kwani sasa tunaweza kurahisisha mawasiliano yetu.

Comments

Popular posts from this blog

JUHUDI ZA MWALIMU NYERERE KATIKA KUKUZA NA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII NCHINI