Baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha kuwataka waandishi wote wa habari za kiuchunguzi pamoja na watafiti kuweka hadharani na kuueleza umma kile kilichotokea Zanzibar, Waandishi na watafiti mabalimbalai wamejitokeza na vielelezo vinavyoeleza jinsi uchaguzi huo ulivyoharibika Vielelezo hivyo ni Nakala za fomu namba MUR. 12A za matokeo zilizotoka katika vituo vya kujumuisha kura ambazo zilikuwa zimejazwa kimakosa. Hii ni fomu kutoka Kituo cha Skuli ya Mabaoni namba 23801 , Jimbo la Chonga namba 2909 fomu hii siyo halali kutokana na kukosa mhuri wa tume ya uchaguzi Zanzibar. Msimamizi wa kituo ni Khamis mkungwa Zaid. Fomu nyingine inatoka katika kituo cha Urusi chenye namba 26503, katika jimbo la Jang’ombe namba 1940 A. Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008 Hii ni fomu kutoka kituo cha Gamba namba 2008, Jimbo la Mkwajuni namba 1926, fomu hii imepoteza uhalali kwasababu imefutwafutwa na haina...
Wachezaji wa Timu ya TTPL na Polisi Moro wakiwania mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Muungano zinazofanyika katika viwanja vya Gymkhana Zanzibar timu ya Polisi Moro imeshinda 36--33. Mchezaji wa timu ya TTPL Mwanaasha Ali ( GS) akiwa na mpira huku mchezaji wa timu ya Polisi Moro Jawa Iddi (GD) akijiandaa kumzuiya katika mchezo wao wa kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu ya Muungano ya Mchezo wa Netiboli yanayofanyika katika viwanja vya Gmykhana Zanzibar Timu ya Polisi Moro imeshinda 36--33. Kocha wa Timu ya TTPL akitowa maelezkezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya kota ya tatu timu hizo zikiwa sare ya 25-25 Kocha wa Timu ya Polisi Moro akitowa maelezkezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko ya kota ya tatu timu hizo zikiwa sare ya 25-25 Mchezaji wa Timu ya Polisi Moro Maryam Shabani (GS) na wa Timu ya TTPL Hawa Pembe wakiwania mpira. Semeni Aswile(WD) akidaka mpira katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Muungano mchezo uliofanyika uwanj...
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU GHARAMA ZA MATIBABU YA DAWA YA SUMU YA NYOKA NCHINI Kama tunavyofahamu, nchi yetu ina aina mbalimbali za nyoka ambao pindi wakimuuma mtu huleta madhara mbalimbali ya kiafya. Aidha tunafahamu kwamba tatizo hili lipo zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uwezo wa wananchi kumudu gharama za matibabu ni mdogo. Dawa za kutibu sumu ya nyoka huagizwa kutoka nje ya nchi. Dawa hizo siyo tu hazipatikani kwa urahisi, bali pia zinapatikana kwa gharama kubwa. Bei ya kununulia dawa hizi ni kati ya dola za kimarekani 55 hadi 85 (yaani shilingi za kiTanzania 118,250 hadi 182,750) kwa kichupa kidogo (vial) kimoja. Kichupa hicho huweza kutumika kwa wagonjwa wanne, lakini mara tu baada ya kufunguliwa dawa hiyo huwa haifai tena kutumika ndani ya mwezi mmoja tu. Pamoja na changamoto hizo, Serikali kupitia MSD kila mwaka huagiza dawa hizi kwa ajili ya mahitaji hayo ya kutibu wagonjwa walioumwa na nyoka, ambapo bei ya kuinunua kutoka MSD ni TZS 200,000/= kwa kichupa kim...
Comments
Post a Comment