Dk.Hussein Ali Mwinyi amewatembelea Wafanya Biashara wa Kijangwani Zanzibar
18 Nov 2020
Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Hassan Khatibu Hassan (katikati) alipokuwa akitoa maelezo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi kuhusu Mradi wa katika Eneo la Soko la Kijangwani Wilaya ya Mjini kabla Rais, kuzungumza na Wajasiriamali wadogo wadogo katika Soko hilo leo akiwa katika ziara ya Kikazi kujuwa Changamoto mbali mbali zinazowakabili Wafanyabiashara hao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Hassan Khatib Hassan wakati alipowasili katika Soko la Wajasiriamali wadogo wadogo Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo Changamoto mbali mbali zinazowakabili
Baadhi ya Wafanyabiashara ndogo ndogo wakimsiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati alipozungumza nao na kuwataka kuwana subira wafanyiwe maamuzi sahihi ya kupatiwa Eneo jengine la kufanyika Biashara zao kwa uhakika,aliyasema hayo leo katika soko la Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwapungia mkono Wafanyabiashara Ndogo Ndogo katika Soko la Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara ya Kikazi kujuwa changamoto mbali mbali kwa Wafanaybishara hao
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mhe.Hassan Khatib Hassan wakati alipowasili katika Soko la Wajasiriamali wadogo wadogo Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo Changamoto mbali mbali zinazowakabili
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati alipokuwa akizungumza na Wajasiriamali wadogo wadogo katika Soko la Kijangwani Wilaya ya Mjini Mkoa wa Mjini Magharibi leo alipofanya ziara ya kujuwa Changamoto mbali mbali zinazowakabili wafanyabiashara hao
Comments
Post a Comment