Posts

Showing posts from November, 2016
Image
BALOZI SEIF AKABIDHI MCHANGO WAKE ALOAHIDI KUCHANGIA UJENZI WA JENGO LA SITI BINT SAAD. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kulia akimkabidhi mchango wa shilingi Milioni 3,000,000/- Msaidizi Katibu wa Taasisi ya  Kumbu kumbu ya Siti Binti Saad Bwana Mohammed Suleiman Omar hapo Ofisini kwake ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.   Ahadi hiyo aliitoa wakati wa hafla maalum ya kuichangia Taasisi ya Kumbukumbu ya Siti Binti Saad iliyofanyika kwenye Hoteli ya Park Hyatt Mjini Zanzibar miezi Miwili iliyopita ambapo Mgeni Rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein.( Picha na – OMPR –ZNZ.)   Na. Othman Maulid. OMPR.  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  alisema Visiwa vya Zanzibar  vitaendelea kupata heshima Kimataifa kadri siku zinavyoaidi kuyoyoma katika Nyanja ya sanaa na utamaduni kufuatia kazi kubwa iliyokuwa ikifanywa  na Msanii mkongwe
Image
RAIS WA ZANZIBAR DK SHEIN, AZUNGUMZA NA MWAKILISHI WA UNICEF Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mwakilishi wa   UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na  Mwakilishi wa   UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mwakilishi wa   UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman (wa pili kulia) alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Mwakilishi wa   UNICEF katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ms. Maniza S.Zaman baada ya mazungumzo yao alip

RC SINGIDA AAHIDI KUREJESHA SHAMBA LA SAGARA LENYE EKARI ZAIDI YA ELFU TANO KWA WANANCHI

Image
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa watu kijiji cha Sagara na vijiji jirani juzi. Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe ameagiza wakazi wa kijiji cha Sagara watumie shamba linalomilikiwa na halmashauri ya Singida bila kubughuziwa wakati anaendelea na taratibu ya kufuta umiliki wa shamba hilo na halamshauri ya wilaya ya Singida. Mbunge wa jimbo la Singida kaskazini Mhe. Lazaro Samwel Nyalandu akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na umati mkubwa wa kijiji cha Sagara kata ya Ngimu. Pamoja na mambo mengine Mhe Nyalandu aliiomba serikali ingalie uwezekano wa kuwakabidhi wananchi wa kijiji cha Sagara shamba lenye ukubwa wa ekari 5,430 ambalo halmashauri ya wilaya ya Singida imeshindwa kuliendeleza . Mwenyekiti wa CCM Mkoa na mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida Martha Mlata akitoa nasaha zake kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Sagara ulioitishwa na Mkuu wa mkoa wa Singi

MPE MTOTO WAKO NAFASI YA KUTIMIZA NDOTO YAKE

Image
Ni vizuri kumpa nafasi mtoto wako kuonyesha kipaji chake kuanzia chini na kumuandaa kutimiza ndoto zake,Muda ni kuanzia saa nne asubuhi viwanja Shaban Robert  Upanga.

MAGAZETI YETU LEO,NOV 30

Image
TANZANIA UK
Image
RAIS DKT MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA GEREZA LA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM LEO,PIGA MARUFUKU UUZWAJI WA SARE ZA MAJESHI KWA WATU BINAFSI        Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kitabu cha wageni akiwa na  Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipewa muhtasarai wa kazi  na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja kabla ya kuongea na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam leo Novemba 29, 2016   Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikaribishwa na Kamishna Mkuu wa Magereza John Casmir Minja ili aongee  na maafisa na askari wa Jeshi la Magereza alipofanya ziara ya kustukiza katika Gereza la Ukonga jijini Dar es salaam