Posts

Showing posts from January, 2018

CCM KIBAHA MJINI YAKAMIA KUUZIKA UPINZANI UCHAGUZI 2019/2020

Image
  Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda (mwenye kofia) akishirikiana na wajumbe wa jumuiya hiyo kufyeka katika mazingira ya jengo la chama hicho wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 41 ya chama hicho wilayani Kibaha leo,yaliyofanya na jumuiya ya wazazi Mjini hapo   Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wazazi Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda (mwenye kofia) akishirikiana na wajumbe wa jumuiya hiyo kuzoa takataka na kuweka katika vifaa vya kubebea uchafu katika mazingira ya jengo la chama hicho wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 41 ya chama hicho wilayani Kibaha leo,yaliyofanywa na jumuiya hiyo.(picha na Mwamvua Mwinyi) Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha,Maulid Bundala (katikati) akikabidhi kadi ya CCM kwa Aliyekuwa Mgombea wa udiwani kupitia Chama cha Wananchi (CUF) 2015,kata ya Kongowe ,Mathas Kambi (anaepokea kadi) baada ya jumuiya ya wazazi CCM Wilaya ya Kibaha kufanya usa
Image
RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA UHAMIAJI MTANDAO NA PASIPOTI MPYA YA TANZANIA YA KIELEKTRONIKIA Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 31 Januari, 2018 amezindua mfumo wa uhamiaji mtandao (e-Immigration) ambao utasaidia kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi, kudhibiti ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali na kuimarisha utoaji wa huduma za kiuhamiaji kwa raia wa Tanzania na wageni wanaoingia na kuishi hapa nchini kwa madhumuni mbalimbali. Uzinduzi wa mfumo huo umefanyika katika ofisi kuu ya uhamiaji Jijini                 Dar es salaam na kuhudhuriwa na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti     wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Seif Ali Iddi, na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa. Wengine ni Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Jaji Mkuu    wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu, Spika