Posts

Showing posts from May, 2019

RAIS DKT MAGUFULI AREJEA NCHINI AKITOKEA AFRIKA KUSINI, NAMIBIA NA ZIMBABWE

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alifanya ziara rasmi ya siku mbili kwa kila nchi.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Kamishna wa Polisi Diwani Athumani baada ya kutelemka kutoka katika ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo alhamisi Mei 30, 2019 akitokea Afrika Kusini alikohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa nchi hiyo Mhe. Cyril Ramaphosa kabla ya kuelekea nchini Namibia na Zimbabwe ambako alif

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MWANAMWEMA SHEIN, AJUMUIKA NA WATOTO YATIMA WA MAZIZINI ZANZIBAR KATIKA FUTARI ALIYOWAANDALIA

Image
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akiwa na Mtoto anayelelewa katika Nyumba ya Watoto Mazizini Zanzibar Mtoto Nadir Abdalla mwenye umri wa mwaka moja na miezi mitano,baada ya kumalizika kwa hafla hiyo ya futari maalum aliyowaandalia katika makazi yao mazizini Zanzibar. Watoto wa Nyumba ya Watoto Mazizuini Zanzibar wakiwa katika futari ilioandaliwa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, iliofanyika katika makazi yao mazizini Zanzibar. Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, akijumuka na Watoto wa Nyumba ya Watoto Yatima Mazizini Zanzibar katika Futari Maalum aliyowaandalia jana 28-5-2019, katika makazi yao mazizini, akiwa na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi.

NCHINI NAMIBIA KUMENOGA KISWAHILI NDIO LUGHA YETU

Image

ANGA YETU MALI YETU USAFIRI WETU

Image

Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha nyama cha kampuni Meatco kilichopo Jijini Windhoek

Image
Mhe. Rais Magufuli ametembelea kiwanda cha nyama cha kampuni Meatco kilichopo Jijini Windhoek na kuelezwa na Kaimu Mtendaji Mkuu wa kiwanda hicho Bw. Jannie Breytenbach kuwa kiwanda kina uwezo wa kuchinja ng’ombe 630 kwa siku, kimeajiri wafanyakazi 650 na kwamba kampuni hiyo ipo tayari kushirikiana na Tanzania kuanzisha viwanda vya nyama.  Mhe. Rais Magufuli amesema Tanzania ni nchi ya pili kwa idadi kubwa ya mifugo Barani Afrika na ameikaribisha kampuni ya Meatco kuja kuwekeza nchini Tanzania.  Katika ziara hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameongozana na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi. 

MAKAMU WA RAIS KUFUTURISHA WANANCHI WA PEMBA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na baadhi ya Viongozi na Wananchi alipowasili Uwanja wa Ndege wa Karume Kisiwani Pemba Leo May 29,2019, kwa ajili ya kufutarisha Wananchi wa Pemba.

RAIS MAGUFULI AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA RAIS WA ZIMBWABWE NA KUSHIRIKI DHIFA YA KITAIFA ILIYOFANYIKA IKULU JIJINI HARARE.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa inayoonyesha baadhi ya Wanyama waliopo katika Hifadhi mbalimbali za Wanyama Tanzania pamoja kabla ya kuanza mazungumzo katika Ikulu ya Harare Zimbabwe. Mei 28, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa kwa Dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa Ikulu ya Harare nchini Zimbabwe. Mei 28, 2019. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati wa Dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa na Mwenyeji wake Rais wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa Ikulu ya Harare nchini Zimbabwe. Mei 28, 2019.

RAIS DKT MAGUFULI APOKEWA NA RAIS DKT HAGE GEINGOB IKULU YA NAMIBIA

Image

RAIS WA TANZANIA ALIPOTOA HESHIMA KWA MASHUJAA NCHINI NAMIBIA

Image

IMF ILIPOKILI KUHUSU TAARIFA ZAKE ZA MAGUMASHI JUU YA UCHUMI WA TANZANIA

Image

DUA YA SHEIKH KIPOZEO

Image

NCHI YETU IMEBARIKIWA KILA KITU

Image

RAIS MAGUFULI AWASILI NCHINI ZIMBABWE KWA ZIARA RASMI YA KITAIFA YA SIKU 2

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 28 Mei, 2019 amewasili katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe ambapo amepokelewa na mwenyeji wake mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  tarehe 28 Mei, 2019 amewasili katika Jiji la Harare nchini Zimbabwe ambapo amepokelewa na mwenyeji wake mwaliko wa Rais wa Zimbabwe, Mhe. Emmerson Mnangagwa. Mhe. Rais Magufuli atakuwa na mazungumzo ya falagha na mwenyeji wake, Mhe. Rais Munangagwa na kisha atahudhuria Dhifa ya Kitaifa iliyoandaliwa na Mhe. Rais Mnangagwa kwa heshima yake. Mhe. Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake na kisha atatembelea na kuweka shada la maua katika eneo la mashujaa wa ukombozi wa Zimbabwe. Katika ziara hii Mhe. Rais Magufuli ameongozana na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) Tanzania Bara Ndg. Philip Mangula, Waziri wa Mambo ya Nje

RAIS MAGUFULI PAMOJA NA RAIS WA NAMIBIA WAZINDUA MTAA WA JULIUS K. NYERERE KATIKA JIJI LA WINDHOEK NCHINI NAMIBIA.

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimweleza Mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob alichokiandika kwenye kitabu cha kumbukumbu kwa Lugha ya Kiswahili Katika kuhakikisha Kiswahili kinatangazwa kimataifa mara baada ya kuwasili katika Ikulu ya Jijini Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahi na mwenyeji wake Rais wa Namibia Mheshimiwa Dkt. Hage Geingob wakati wa hafla ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia. Mei 27, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapongeza Watanzania wanaoishi Namibia mara baada ya kuzindua mtaa mpya wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius K. Nyerere unaoitwa JULIUS K. NYERERE uliopo katika Jiji la Windhoek Nchini Namibia.Mei 27, 2019 Rais wa Jamhuri ya Muunga