Posts

Showing posts from June, 2022

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AHUTUBIA KWENYE KILELE CHA SHEREHE YA MIAKA 25 YA MFUKO WA FURSA SAWA KWA WOTE (EOTF) JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia katika kilele cha Sherehe ya miaka 25 ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo tarehe 27 Juni, 202 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti wa Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) Mama Anna Mkapa pamoja na Baadhi ya Wake wa Viongozi mara baada ya kuwasili kwenye ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere JNICC Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilele cha maadhimisho ya miaka 25 ya Mfuko huo tarehe 27 Juni, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu H

BALOZI MULAMULA ATAKA MIGOGORO KATIKA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA IMALIZWE

Image
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika kiti cha Tanzania wakati wa Mkutano  wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika nchini Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Mawaziri wenzake  wanaoshiriki katika mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika nchini Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa na makabrasha ya mkutano akilekea kwenye Kiti cha Tanzania kwa ajili ya kushiiki mkutano wa Mawaziri wa s Jumuiya ya Madola unaofanyika nchini Rwanda. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akihojiwa na mwandishi wa Kituo cha Runimga cha Channel 10, Bw. Ezekiel Mwamboko. Aliyemshikia kipaza sauti ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika  Wizara ya Mambo

MRADI WA SH. 540 MILIONI KUONDOA KERO YA MAJI KWA WANANCHI MANISPAA YA SINGIDA

Image
Mkuu wa Wilaya ya Singida Mhandisi Paskas Mulagiri akiangalia mtambo wa kuchimba Visima vya Maji wa  Kampuni ya N & Ground Water Tanzania LTD ya Dodoma ulivyokuwa ukichimba kisima cha mradi wa  Maji Kata ya  Mwankoko uliopo nje kidogo ya Manispaa ya Singida wakati alipotembelea mradi huo jana unaotekelezwa kwa fedha za UVIKO- 19. Mkurugenzi Mtendaji wa SUWASA Mkoa wa Singida Sebastian Warioba akielezea utekelezaji wa miradi ya maji ya eneo la Mwankoko na Kata ya Unyambwa. Kulia ni Meneja Biashara wa SUWASA Mkoa wa Singida, Hosea Maghimbi na kushoto ni Afisa Ugavi wa SUWASA , Michael Salema. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya N & Ground Water Tanzania LTD ya Dodoma iliyopewa zabuni ya kuchimba kisima kimoja cha mradi huo eneo la Mwankoko, Mhandisi Naftal akielezea uchimbaji wa kisima hicho ambapo pia aliishauri Serikali kuwatumia wakandarasi waliosajiliwa na Wizara na wenye uzoefu wa kazi hiyo.

JAMII YA WAWINDAJI YA WAHADZABE SINGIDA WAIPONGEZA SERIKALI KWA KUWAPIMIA ARDHI

Image
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula akimpatia hatimliki ya kimila Bibi Agnes Mangashini kutoka Jamii ya Wawindaji ya Wahadzabe wa Kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza wilayani Mkalama wakati wa hafla ya kukabidhi hati hizo iliyofanyika jana.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Sophia Kizigo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula akizungumza katika hafla hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Mkalama ,Sophia Kizigo akizungumza wakati wa zoezi la utoaji hatimiliki hizo. Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dk.Angeline Mabula na Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Sophia Kizigo (kushoto)  wakiserebuka na Wanawake wa Kikundi cha Sanaa cha Jamii ya Wawindaji ya Wahadzabe wa Kijiji cha Munguli Kata ya Mwangeza wilayani Mkalama. Watoto wakiwa kwenye hafla hiyo.

WAZIRI DKT MABULA AIPONGEZA JAMII YA WAHADZABE KWA KUKUBALI KUPIMIWA ARDHI

Image
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula ameipongeza jamii ya wawindaji ya wahadzabe iliyopo wilaya ya Mkalama mkoani Singida kwa utayari iliyouonesha wa kutambua na kukubali kupimiwa maeneo yao na kupatiwa hatimiliki za kimila. Jumla ya hatimiliki za kimila mia moja (100) zikiwemo 26 zinazomilikiwa kwa pamoja kati ya mke na mume zimetolewa kwa jamii ya wawindaji ya Wahadzabe ikiwa ni hatua kubwa kutokana na jamii hiyo kujishughulisha zaidi na uwindaji, utafutaji matunda, urinaji asali na uchimbaji mizizi. Dkt Mabula alisema, hatua hiyo inaonesha nia na dhamira njema waliyonayo ya kutaka kuyalinda maeneo yao wenyewe na kwa kushirikiana na serikali. ‘’Hakika hizi ni salamu na ujumbe wa Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa jamii ya wawindaji inaungana naye na mkoa tayari kwenda naye sambamba katika kuletea watu wote maendeleo’’ alisema Dkt Mabula. Akizungumza na wananchi wa jamii ya wawindaji ya Wahadzabe katika kijiji cha Mungu

RAIS SAMIA AWASILI MUSCAT NCHINI OMAN KWA AJILI YA ZIARA YA KIKAZI YA SIKU TATU

Image
Kikosi cha Jeshi la Oman kikiwasili katika viwanja vya Kasri ya Al Alam kwa ajili ya Mapokezi Rasmi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Muscat nchini Oman tarehe 12 Juni, 2022.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Mwenyeji wake Kiongozi Mkuu wa Taifa la Omani Sultan Haitham bin Tariq Al Said wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa katika mapokezi Rasmi yaliyofanyika kwenye viwanja vya Kasri ya Al Alam Muscat nchini Oman tarehe 12 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Kiongozi Mkuu wa Taifa la Omani Sultan Oman Haitham bin Tariq Al Said kabla ya kuanza mazungumzo yaliyofanyika Kasri ya Al Alam Muscat nchini Oman tarehe 12 Juni, 2022.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Oman mara baada ya kuwasili Kasri ya Al Alam Muscat nchini humo ta

Siku ya Kwanza ya Ziara ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Kagera Tarehe 08 Juni, 2022

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wananchi wa Kata ya Bwanga Wilaya ya Chato Mkoani  Geita alipokua njiani akielekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu inayoanza tarehe 08 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi na Wananchi wa Mkoa wa  Geita alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Geita alipokuwa akielekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu inayoanza tarehe 08 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Wasanii wa Vikundi vya ngoma mbalimbali alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Geita, alipokuwa akielekea Mkoani Kagera kwa ajili ya kuanza ziara ya kikazi ya siku tatu inayoanza tarehe 08 Juni, 2022. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisalimiana na Viongozi pamoja na Wananchi wa Biharamulo Stand alipowasili Mkoani  Kagera kwa ajili ya kuanza z

Kamati ya GFT yakagua maendeleo ya Mradi wa JNHPP, yaipongeza serikali

Image
Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) imeipongeza serikali kwa kupiga hatua zaidi katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo. Pongezi hizo zimetolewa na Meneja Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TAZARA) Mhandisi Fuad Abdallah kwa niaba ya wajumbe wote wa GFT wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo inayofanyika katika maeneo tofauti ya mradi huo, kuanzia June 6-11, mkoani Pwani.  Mhandisi Fuad alisema kuwa wamefanya ziara hiyo kwa kukagua maeneo mbalimbali ya mradi huo ambapo walikagua maendeleo ya ujenzi wa Tuta kuu la Bwawa, Kituo cha Kuchochea Umeme, Nyumba ya kuendeshea Mitambo ya kuzalisha umeme na Kingo za Bwawa (Saddle Dam) Muonekano wa eneo la kupeleka maji katika mitambo ya kufua umeme katika mradi wa JNHPP, Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT)walifa nya ziara ya kukaua eneo hilo Jun