Posts

Showing posts from February, 2017

MAKALA: WIKI YA SHERIA NA SIKU YA SHERIA NCHINI, 2017

Image
Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Juma akikagua gwaride maalum lililoandaliwa, ukaguzi wa gwaride hili huashiria kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama kwa mwaka husika. Na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania Nchi yoyote yenye kuzingatia misingi ya Utawala wa Sheria, huchangia kwa kiasi kikubwa kuleta amani na Maendeleo ya kiuchumi katika taifa husika. Hii inajidhihirisha kupitia Kaulimbiu ya Wiki ya Sheria na Siku ya Sheria nchini, 2017 ambayo ni ‘Umuhimu wa Utoaji Haki kwa wakati kuwezesha Ukuaji wa Uchumi.’ Kauli mbiu hii ina maana ya kuwa kukamilishwa mapema kwa mashauri ya jinai, Rushwa na Uhujumu Uchumi ambayo yanaendeleza amani na usalama katika jamii ni chachu ya maendeleo ya uchumi. Hivi karibuni Mahakama ya Tanzania iliadhimisha Siku ya Sheria nchini, ambayo huashiria kuanza rasmi kwa mwaka wa Mahakama ambapo shughuli za usikilizaji wa Mashauri huanza rasmi. Kwa mwaka huu, sherehe za Siku ya Sheria nchini ziliadhimishwa rasmi tarehe 02.02.20
Image
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU VIFUNGASHIO VYA POMBE KALI – VOROBA Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Mamkamba. (MB) akitoa Taarifa kwa Umma kuhusu marufuku ya uzalishaji, uingizaji , usambazaji,na matumizi ya vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba vinavyotumika kufungashia pombe kali, alipozungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Mtaa wa Luthuli Jijini Dare es Salaam Leo. Katikati Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. (MB) akitoa Taarifa kwa Umma kuhusu marufuku ya uzalishaji, uingizaji , usambazaji,na matumizi ya vifungashio vya plastiki maarufu kama viroba vinavyotumika kufungashia pombe kali, kulia ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Profesa Faustin Kamuzora na Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Mazingira, Waziri Makamba alizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake mtaa wa Luthuli Jijini Dare es Salaam Leo. Mtakumbuka tarehe 20 Februari 2017 Ofisi ya Makamu wa Rai

MAGAZETI YA LEO JUMANNE

Image
Image
Mawaziri wa Zanzibar watembelea Wizara ya Ardhi ya SMT kwa ajili ya kubadilishana uzoefu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akiwaelezea Mawaziri kutoka Zanzibar jinsi Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kinavyorahisisha kutoa Huduma za Ardhi bila usumbufu kwa Wananchi.  Kuanzia Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud, Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Mhe. Hamad Rashid, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira Zanzibar Mhe. Salama Talib na Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Dkt. Yamungu Kayandabila. Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe William Lukuvi akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud jinsi ya kutumia mashine ya kutolea huduma za Ardhi katika kituo cha Huduma kwa Mteja cha Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na M