Posts

Showing posts from May, 2022

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKIPOKEA TUZO YA BABACAR NDIAYE

Image
  Rais   @ SuluhuSamia   akipokea Tuzo ya Babacar Ndiaye kwa mwaka 2022 kutoka kwa Makamu wa Rais wa Sekta Binafsi, Miundombinu na Viwanda kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Solomon Quaynor kwa niaba ya Rais wa Benki hiyo Dkt. Akinumwi Adesina. Hafla ya Utoaji wa Tuzo hiyo imefanyika kwenye siku ya pili ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa AfDB, Accra nchini Ghana tarehe 25 Mei, 2022.

CCM YAWASILISHA MAONI NA MAPENDEKEZO YA CHAMA KUHUSU MASUALA YANAYOHUSU DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI VYA SIASA.

Image
Katibu  Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo amewasilisha maoni na mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi kwa Kikosi Kazi Cha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kinachofanyia kazi masuala yanayohusu Demokrasia ya Vyama Vingi vy Siasa leo tarehe 24, Mei 2022 katika ukimbi wa ofisi ndogo ya Bunge jijini Dar es Salaam. Katika kikao hicho cha kuwakilisha maoni na mapendekezo ya Chama Cha Mapinduzi, Katibu Mkuu Chongolo aliongozana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Unenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka.