Posts

Showing posts from January, 2017
Image
BOTI YA MIZIGO NA ABIRIA SITA YADAIWA KUPOTEA ZIWA TANGANYIKA,ILIKUWA IKITOKA KIGOMA KWENDA CONGO. Na Rhoda Ezekiel Kigoma. BOTI ya mizigo iliyokuwa ikitokea Kigoma kuelekea Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ya Kalemi, imepotea katika ziwa Tanganyika ikiwa na Watu sita pamoja na Shehena ya vitungu gunia 110, ngano mifuko180 ,Mafuta ya taa dumu 20 na kreti za soda 70  ambayo mpaka sasa haijulikani ilipo. Akizungumza na Wanahabari Mkoani humo kamanda wa polisi  Mkoa wa Kigoma Fredinandi Mtui alisema Mnamo tarehe 23 januari majira ya saa 16:30 jioni boti iliyotengenezwa  kwa mbao MV.Ngendo ya Buchuma, boti ya mizigo inayo milikiwa na  Mussa Hamisi Mkazi wa ujiji Kigoma Manispaa ,iliondoka  Katika Bandari ya Kibirizi ikiwa na shehena ya vitunguu, Ngano na watu sita kuelekea Congo ambayo mpaka sasa haijafika Congo na haijulikani ilipo. Mtui alisema mpaka sasa boti hiyo haijulikani ilipo na hakuna chochote kilicho onekana kati ya mizigo wala abiria Waliokuwa wamepanda katika boti hilo,

SERIKALI YAELEZA UTEKELEZAJI WA MASUALA MBALIMBALI BUNGENI

Image
Dodoma, Jumanne, Januari 31, 2017:     Serikali leo imeainisha utekelezaji na kutoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi katika sekta mbalimbali katika kikao cha kwanza cha Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majibu ya Serikali kwa baadhi ya hoja ni kama ifuatavyo:                           Ujenzi Nyumba za Walimu. Akijibu hoja kuhusu ujenzi wa nyumba za walimu, Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo, ameliambia Bunge kuwa Serikali ilitenga kiasi cha Sh. Bilioni 13.9 katika Bajeti ya mwaka huu kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu wa Sekondari, na Shilingi bilioni 11.4 kwa nyumba za walimu wa Shule za Msingi. Aidha, Waziri Jafo ameeleza kuwa tayari nyumba 146 za walimu zimeshajengwa nchini kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari. Pia amezungumzia Serikali kuanza kulipa madeni ya walimu.                              Ujenzi wa Viwanda Nchini Akijibu swali ku
Image
SHIRIKISHO VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM, LAWATAKA VIJANA KUZIDISHA UADILIFU NA UZALENGO KUKIDHI LENGO LA RAIS DK. MAGUFULI Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu, Daniel Zenda akizungumza wakati wa kufungwa Kambi ya Vijana 219,  waliokuwa katika kambi ya kukuza Uzalendo, iliyowekwa Hombolo mkoani Dodoma. Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu nchini, limewahimiza Vijana kuzidisha uadilifu na uzalendo ili kufikia malengo yatakayoakisi CCM mpya na Tanzania mpya, kama anavyotaka Mwenyekiti wa Chama, Rais John Magufuli. "Ili matakwa haya ya Rais wetu na Mwenyekiti wa Chama, yaweze kufikika, ni lazima  Watanzania  hasa sisi vijana, tubadilike, kifikra na kimtazamo na kuacha kufanya kazi kwa mazoea", alisema Kaimu Katibu Mtendaji wa Shirikisho hilo, Daniel Zenda, wakati wa kufungwa kambi maalum ya siku tatu ya Vijana kutoka  vyuo mbalimbali, nchini, jana, Hombolo, mkoani Dodoma. Zenda alisema, mabadiliko ya kifikra, mtazamo na kiutendaji, ndivyo vitaka
Image
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi kabla ya kuanza maz

MWITONGO LIWE ENEO TENGEFU LA KIHISTORIA NA UTALII NCHINI - BALOZI AMINA

Image
  Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Balozi Amina Salim Ali (mwenye suti nyeusi)akiwa na viongozi wa mkoa wa Simiyu watembelea kaburi la Hayati Baba wa Taifa wilayani Butiama leo.   Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Balozi Amina Salim Ali (mwenye suti nyeusi)akiwa na viongozi wa mkoa wa Simiyu wakitembelea maeneo tofauti katika makazi ya Hayati Baba wa Taifa wilayani Butiama leo. Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar, Mhe Amina Salum Ali ameyasema hayo leo  alipotembelea makazi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere wilayani Butiama. "Serikali iwekeze katika uhifadhi wa historia ya Tanzania na kurahisisha utaratibu wa wananchi kutembelea makumbusho ya Mwitongo ili kupata taarifa sahihi zinazoeleza kwa kina historia ya Taifa letu," alisema Balozi. Balozi Amina alisisitiza kuwa hiyo ilikuwa fursa adhimu sio tu ya kuongeza pato la utalii, bali pia katika kuwarithisha watoto wa Tanzania historia ya n

MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA PALESTINA JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat, Ikulu jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kitabu alichokabidhiwa na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat, Ikulu jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Palestina nchini Mhe. Hazem M.Shabat (kushoto) mara baada ya kumaliza mazungumzo, Ikulu jijini Dar es Salaam.

MAGAZETINI LEO

Image