Posts

Showing posts from October, 2022

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKAGUA MABEHEWA YA TRENI YA RELI YA SGR YA SHIRIKA LA RELI TANZANIA,YANAYOTENGENEZWA NCHINI KOREA KUSINI

Image
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja ya mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo yanatengenezwa katika kiwanda cha kampuni ya Sung Shin Rolling ya Korea. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo ametembelea kiwanda hicho na kujionea maendeleo ya utengengenezaji wa mabehewa hayo, Oktoba 25, 2022. Wengine pichani kutoka kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Korea, MheTogolani Idrissa  Mvura, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mabarouk,  Rais na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni yaSung Shin Roliing, BW. Gye Shul Park na kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Emmanuel Tutuba. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa ndani ya moja ya mabehewa ya Reli ya Kisasa (SGR) ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambayo yanatengenezwa katika kiwanda cha kampuni ya Sung Shin Rolling ya Korea. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika ziara ya kikazi nchini humo ametembelea kiwanda

RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO MHE. FÉLIX ANTOINE TSHISEKEDI TSHILOMBO AWASILI TANZANIA APOKEWA NA MWENYEJI WAKE RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

Image
Rais @SuluhuSamia akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022. Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 2 Jijini Dar es Salaam tarehe 23 Oktoba, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakati wa Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukipigwa mara baada ya Rais huyo wa DRC kuwasili nchini tarehe 23 Oktoba, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo wakiwa katika

MAONESHO YA 6 YA KIMATAIFA YA UTALII YA KISWAHILI (S!TE) YANAFANYIKA KATIKA JIJI LA KIBIASHARA LA TANZANIA LA DAR-ES-SALAAM

Image
  Tukio hili linaangazia safari za ndani na nje kwenda na ndani ya Afrika. S!TE inalenga kukutanisha wataalamu wengi wa utalii na usafiri kutoka duniani kote. Hafla hii inalenga kutangaza utalii wa Tanzania kwenye masoko ya kimataifa na pia kuwezesha kuunganisha makampuni ya Tanzania, Mashariki na Afrika ya Kati na makampuni ya utalii kutoka sehemu nyingine za Ulimwenguni.  

WIZARA YA UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA KUPITIA TAASISI ZAKE ZA WAKALA WA USAJILI WA BIASHARA NA LESENI (BRELA), TUME YA USHINDANI (FCC) PAMOJA NA KITUO CHA UWEKEZAJI (TIC), WAMEKUTANA NA WADAU MBALIMBALI KUTOKA KATIKA TAASISI ZA UMMA NA BINAFSI

Image
Katika  kikao cha mashauriano kuhusu Itifaki za Ushindani, Uwekezaji na Haki za Miliki Ubunifu, chini ya Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA).  Tanzania ni miongoni  mwa nchi 54 wanachama kati ya nchi 55 za Afrika zilizosaini  makubaliano ya kuanzishwa kwa Eneo Huru la Biashara Afrika, ili kuchochea ukuaji wa uchumi kwa nchi wanachama wa  Afrika. Msajili Msaidizi Mkuu kutoka BRELA Bi. Loy Mhando, akizungumza kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu  Bw. Godfrey Nyaisa, amesema   kikao hicho ni muhimu kwa Taifa na Afrika kwa ujumla kwani kinalenga kutengeneza mazingira rafiki ya ufanyaji biashara katika Eneo Huru la Biashara Afrika ambapo Itifaki hizo ni moja ya suala linalopaswa kuangaliwa kwa jicho la tatu, ili utekelezaji wake utakapoanza wadau waweze kunufaika na bunifu zao pamoja na kuwezesha ufanyaji biashara. Kwa upande wake   Mkurugenzi wa Miungano ya Makampuni,Tafiti na Ushawishi wa Ushindani wa FCC Bi. Zaytun Kikula amewataka wadau kuchangia mawazo yao katika kuboresha chapisho la It

UZINDUZI WA ONESHO LA KIMATAIFA LA UTALII LA SWAHILI (SWAHILI INTERNATIONAL TOURISM EXPO - S!TE, 2022). MLIMANI CITY, DSM MGENI RASMI NI MAKAMU WA RAIS DR. PHILIP ISDOR MPANGO

Image
Lengo kuu la Onesho hili ni kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania, na kukutanisha wanunuzi na wauzaji wa bidhaa za utalii wa Kitaifa na Kimataifa. Onesho hili limehudhuriwa na waoneshaji zaidi 200, wanunuzi wa Kimataifa takribani 100 kutoka masoko ya Kimkakati hususan nchi za Marekani, Uholanzi, Afrika Kusini, India, Urusi, Hispania, UAE, Poland, Finland, Japan, Oman na nyinginezo,Onesho hilo litamalizika tarehe 23 Oktoba 2022