Posts

Showing posts from January, 2023

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIONGOZA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZIRI KILICHOFANYIKA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM.

Image
 

SIASA ZA KIISTARABU ZA RAISI SAMIA NA KUMBUKUMBU YA TUKIO LA " DINNER TABLE BARGAIN 1790 " NCHINI MAREKANI

Image
Ilikuwa Usiku Wa June 20, 1790 Wakati Mikutano Ya " Congress " Inafanyika Jijini Newyork .Thomas Jefferson Wakati Huo Akiwa Secretary Of The State( Baadae Raisi Wa Tatu Wa Marekani) Alipoamua Kuwaalika Chakula Cha Usiku Watu Wawili Alexander Hamilton Wakati Huo Akiwa Secretary Of Treasure  Na James Madison Mwakilishi Wa Jimbo La Virginia( Baadae Raisi Wa Nne Wa Marekani). Ni Majadiliani Katika Kikao Hiki "Dinner Table Bargain Of 1790" Kilichoitishwa Na Jafferson Ndicho Kilicholeta Suluhu Hasa Baada Ya Madison Kukubali Hoja Ya Hamilton Na Kushawishi Majimbo Ya Kusini Kuunga Mkono Hoja Na Kwa Pamoja Kulijenga Taifa Lao Ambalo Leo Ni Moja Ya Mataifa Makubwa Na Yenye Nguvu Duniani. Na Kassim Mpingi  Rufiji-Pwani  Bila Shaka Taifa Linaunganishwa Na Siasa Za Umoja,Mshikamano,Kusameheana Na Kujenga Nchi Kwa Pamoja(4R). Vyama Pinzani Baada Miaka Saba Vinaingia Tena Mtaani Kufanya Mikutano Na Kufurahi Matunda Ya Siasa  Safi Na Za Kiistarabu Za Raisi Samia . Aina Hii Ya Siasa

HOSPITALI YA KISASA KITOGANI,WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAFUNGULIWA NA RAIS MWINYI

Image
 Na Mwandishi wetu Zanzibar Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi afungua Hospitali ya  Kisasa ya Kitogani Wilaya ya Kusini  ,Mkoa wa Kusini Unguja. Kufunguliwa kwa Hospitali hii  pia imeambatana na kufungwa kwa  Vifaa tiba vipya,Gari la kubebea wagonjwa,hospitali ipo tayari kutoa huduma tofauti,ikiwemo huduma za wagonjwa wa nje(OPD),Mama na Mtoto ,huduma za kliniki mbalimbali zikiwemo za Pua,Koo,Masikio ,Macho,Magonjwa yasio ya kuambukiza kama Sukari,shinikizo la damu ,huduma za madawa(pharmacy),huduma za Wagonjwa wanaolazwa ikiwemo ,Wodi za Watoto,Mama Wajawazito kabla na baada ya kujifungua,Watu wazima Wanawake na Wanaume,huduma za wagonjwa wa dharura na ajali,Wagonjwa mahututi(ICU),huduma za watoto njiti ,Wodi tatu za wagonjwa wenye mahitaji maalum ya  kujitenga(isolation) pia Kuna Theatres mbili (2)za kisasa, huduma za ushauri nasaha na kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na huduma za uchunguzi ikiwemo Maabara ,Ultrasound,ECG na XRAYS.K

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ATANGAZA KURUHUSU KUFANYIKA KWA MIKUTANO YA HADHARA KWA VYAMA VYA SIASA NCHINI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kuhusiana na maamuzi ya Serikali ya kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya Hadhara kwa Vyama hivyo wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi wa Vyama Vya Siasa kuhusiana na maamuzi ya Serikali ya kuruhusu kufanyika kwa Mikutano ya Hadhara kwa Vyama hivyo wakati wa Kikao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.   Sehemu ya Viongozi mbalimbali wa Vyama Vya Siasa 19 waliohudhuria Kikao kilichoitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Ikulu Jijini Dar es Salaam Dar es Salaam tarehe 03 Januari, 2023.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa mara baada ya Kikao na Viongozi wa Vyama vya Siasa Ikulu Jijini Dar es Sala

JE UNAJUA DELTA YA RUFIJI NDIO ENEO ZIMEZAMISHWA MELI KUBWA MBILI ZA KIVITA ZA UJERUMANI? SEHEMU YA TANO

Image
  Baadaye Upesi Wajerumani walianza kuondoa silaha kutoka katika manuari hii Königsberg, hizi zilitolewa kwa kamanda wa eneo la Ujerumani, Kanali von Lettow-Vorbeck, ambaye alitumia hizi kuendeleza mapigano katika Afrika Mashariki hadi mwisho wa vita. Takriban mabaharia 33 wa Ujerumani walikufa wakati wa kizuizi na mapigano, wengi wao kutokana na ugonjwa wa kitropiki. Walizikwa kando ya meli. Bamba lililosomeka "Beim Untergang S.M.S. Königsberg am 11.7.15 gefallen..." liliwekwa karibu na makaburi, likiwa na orodha ya waliofariki . German graves alongside the Königsberg.  Picha kwa hisani ya  www.deutsche-schutzgebiete.de Juu na chini: Uharibifu wa Königsberg Juu na chini: Uharibifu wa Königsberg Hali ilivyo sasa Sifa iliyo wazi zaidi ya Delta ya Rufiji ni msitu wake wa mikoko ambao ni mkubwa zaidi nchini Tanzania. Msitu wa mikoko unasaidia mfumo mkubwa wa chakula na delta (na Kisiwa cha Mafia) ni maeneo muhimu ya msimu wa baridi kwa ndege wahamiaji, ikiwa ni pamoja na waders