Posts

Showing posts from May, 2023

KELELE NA MITETEMO INAUWA WATOTO NJITI 12,000 KWA MWAKA ULAYA PEKE YAKE

Image
Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kelele kuwa ni mojawapo ya kisababishi cha madhara katika maisha ya binadamu. Aidha, kwa mujibu wa “European Environmental Agency” (EEA, 2018) kelele zimeainishwa kuwa mojawapo ya visababishi vya vifo vya mapema vya watoto “Pre-mature death” ambapo takwimu zinaonyesha takribani watoto 12,000 hufariki kila Mwaka katika Bara la Ulaya”. Katika nchi yetu changamoto ya kelele zinazozidi viwango vilivyoainishwa na TBS zinatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia. Kwa siku za hivi karibuni, kelele zimeongezeka kwenye maeneo ya kazi na hivyo kusababisha matatizo ya kiafya ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza umakini katika mafunzo, ajali na kupungua uwezo wa kusikilizana. Vyanzo vikuu vya kelele hizi ni kumbi za starehe hasa biashara za vileo (baa), vyombo ya usafiri na usafirishaji (kama magari, ndege na treni), matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwan

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NAMIBIA ‘DIASPORA’

Image
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na baadhi ya Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek tarehe 08 Mei, 2023.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubaloz