FRAVIANA CHALRES - Makamu wa Rais Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS)


Jopo la wanasheria lililokutana Zanzibar kwa siku tatu
 limefurahishwa na juhudi za serikali kuhakikisha nchi iko katika amani
na utulivu kwa kipindi chote cha kampeni na uchaguzi Tanzania

Tumesikia
Mengi toka kila kona hasa kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar Tumekuja na
kujionea wenyewe wananchi wa Zanzibar wanahitaji amani na utulivu kwa
ustawi wa Taifa lao na wanafanya hivyo hakuna kile tulichoaminishwa na
vyombo vya nje kwamba kuna hali tete Zanzibar nimepita kila kona sijaona
hali hiyo pongezi kwa watanzania hawa lakini pongezi kwa serikali pia,
Makamo wa rais wa Chama hicho Fraviana Chalres alifafanua

Alisifu
Juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania kwa kuonyesha moyo
wa dhati kuwa tumikia Watanzania akiwataka wanasheria wote nchini wenye
mapenzi mema na nchi hii kumuunga mkono rais wetu kwa kila hali,tunaomba
kila mwenye uwezo wa kumwombea rais afanye hivyo anapambana na genge
gumu lenye mizizi kila kona

Pia aliitaka Tume
ya Uchaguzi Zanzibar kuzingatia Sheria zilizopo na kukaa na wadau wote
kuumaliza kisheria mzozo wa uchaguzi Zanzibar alimaliza kwa kumwombea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
AMANI NA IDUMU DAIMA

Comments

Popular posts from this blog

JUHUDI ZA MWALIMU NYERERE KATIKA KUKUZA NA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII NCHINI