Mkurugenzi wa Uratibu Shuhuli za Serikali kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Ndg.Khalid
Bakari Amran, akimuonyesha tuta linalojengwa na kaya masikini shehia ya ndagoni
lenye urefu wa mita 200, Naibu waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar
Mhe:Mihayo Juma N’hunga, wa pili kutoka
kulia wakati alipotembelea kukagua kazi zinavyoendelea katika tuta hilo
Hili tuta linalojengwa kwa ajili ya kuzuwia
maji
Chumvi lenye urefu wa mita 200, linalojengwa kwa nguvu kazi za wanakaya
katika bonde la Kidau shehia ya Ndagoni, baada ya kumalizika ujenzi wake
litaweza
kuwarudisha wakulima zaidi ya 300, kuendelea kulima katika mashamba yao
baada ya kuyahama
kwa zaidi ya miaka miwili sasa
Mratibu wa Tasaf Pemba Ndg.Mussa Said, akitoa maelezo ya ujenzi wa Tuta la kuzuwia maji ya Chumvi
lenye urefu wa mita 200, kwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais
Zanzibar Mhe:Mihayo Juma N’hunga, wakati alipotembelea wanakaya wa shehia ya
Ndagoni
Zaidi ya wakulima 300
waliokuwa wakilima mpunga katika bonde la Kidau, wameshindwa kufanya shuhuli
zao za kilimo baada ya bonde hilo kuingia maji Chumvi, ambapo sasa mradi wa
kunusuru kaya masikini unaendelea na ujenzi wa tuta lenye urefu wa mita 200
katika bonde hilo
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe:Mihayo Juma N’hunga, akizungumza na
walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini Shehia ya Ndagoni Kisiwnai Pemba,
katika ziara yake ya siku mbili kisiwani hapa, kuangalia miradi mbali mbali ya
maendeleo inayotekelezwa na Tasaf Pemba
Mkurugenzi wa Uratibu Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Khalid
Bakari Amran, akizungumza na wanakaya masikini shehia ya Ndagoni Wilaya ya
Chake Chake, mara baada ya kukagua kazi za ujenzi wa tuta lakuzuwia maji Chumvi
Mkuu wa Wilaya ya
Chake Chake Pemba Mhe:Salama Mbraouk Khatib, akizungumza na walengwa wa mpango
wa kunusuru kaya masikini Shehia ya Ndagoni, huko katika bonde la Kidau mara
baada ya kumaliza kazi ya ujenzi wa tuta la kuzuwia maji chumvi
Mratibu wa Tasaf Pemba Ndg.Mussa Sadi Kisenge, akitoa ufafanuzi ya fedha kwa wanakaya masikini shehia ya
ndagoni, juu ya ujenzi wa tuta lenye urefu wa mita 200 katika bonde la Kidau
kwa lengo la kuzuwia maji chumvi
Viongozi mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Naibu waziri
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Mhe:Mihayo Juma N’hunga wapili kutoka
kushoto, Mkurugenzi wa Uratibu kutoka ofisi hiyo Zanzibar Mhe;Khalid Bakar
Amran, Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Mhe:Salama Mbarouk Khatib, Afisa Mdhamini
Ofisi ya Makamu wa Pili Salum Ali Matta na katibu Tawala Wilaya ya Chake Chake
Abdalla Rashid.
(Picha na Abdi Suleiman,
PEMBA.
Comments
Post a Comment