UVCCM Wamtembelea na Kumfariji Msanii Ben wa Bongo Movie.
Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa Mhe Sadifa Juma leo ameongoza ujumbe wa viongozi wa
UVCCM kumfariji na kumpa pole msanii wa maigizo ndg Abdul Ahmad jina la
Usanii Ben Serengo nyumban kwao Kigogo Jijini Dar Es Salam, aliyepata
ajali ya gari tareh 25 siku ya skukuu ya Christmas.
UVCCM
inathamini sana mchango wa wasanii wa ndani na inaguswa na changamoto
na matatizo mbali mbali yanayopata wasanii hivyo Jumuiya itaendelea
kuwa nao karibu kwa kuzingatia umuhimu wao katika jamii na Chama Cha
Mapinduzi. Alisema Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mhe:Sadifa Juma
Khamisi(MCC/MB) alipokwenda Kumjulia Hali Msanii wa Bongo Movie Abdul
Ahmad jina maarufu Ben Serengo wa pili kulia na wa tatu kulia ni Kaimu
katibu Mkuu UVCCM Shaka Hamdu Shaka.
Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamisi(MCC/MB) wa nne kulia akitizama
picha mbali mbali za tukio la ajali Msanii wa Bongo Movie Abdul Ahmad
jina maarufu Ben Serengo wa Tatu kulia iliyotokea tareh 25 Siku ya
Skukuu yaChristmas.
Mwenyekiti
wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamisi(MCC/MB) wa Tatu kushoto akizungumza
na mama wa msanii Bi Jasmin Rajabu Hatia Mara baada ya kutoka kumuona
mgonjwa.
Comments
Post a Comment