MWITONGO LIWE ENEO TENGEFU LA KIHISTORIA NA UTALII NCHINI - BALOZI AMINA



 Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Balozi Amina Salim Ali (mwenye suti nyeusi)akiwa na viongozi wa mkoa wa Simiyu watembelea kaburi la Hayati Baba wa Taifa wilayani Butiama leo.
 Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko wa Zanzibar, Balozi Amina Salim Ali (mwenye suti nyeusi)akiwa na viongozi wa mkoa wa Simiyu wakitembelea maeneo tofauti katika makazi ya Hayati Baba wa Taifa wilayani Butiama leo.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Zanzibar, Mhe Amina Salum Ali ameyasema hayo leo  alipotembelea makazi ya Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere wilayani Butiama.

"Serikali iwekeze katika uhifadhi wa historia ya Tanzania na kurahisisha utaratibu wa wananchi kutembelea makumbusho ya Mwitongo ili kupata taarifa sahihi zinazoeleza kwa kina historia ya Taifa letu," alisema Balozi.

Balozi Amina alisisitiza kuwa hiyo ilikuwa fursa adhimu sio tu ya kuongeza pato la utalii, bali pia katika kuwarithisha watoto wa Tanzania historia ya nchi yetu.

Waziri Amina ametoa wito kwa wananchi kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano ili kuendeleza Muungano ulioasisiwa na Baba wa Taifa pamoja na Hayati Mzee Sheikh Abeid Aman Karume.

Mh Balozi amepata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali katika makazi hayo.

Waziri Amina Salum Ali amefanya ziara wilayani Butiama akitokea mkoani Simiyu ambako alifanya ziara ya siku tatu iliyokuwa na lengo la kutembelea na kuona maeneo mbalimbali yanayohusu sekta ya viwanda na biashara mkoani humo.

Naye Mwenyezi wake,  Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mh Anthony Mtaka, aliyekuwa ameambata na Balozi Amina, ametoa rai kwa viongozi hapa nchini kumuenzi kwa vitendo Hayati Baba wa Taifa kwa kuendeleza mema aliyoyaanzisha kwa maslahi ya wananchi naTaifa kwa ujumla.

"Viongozi na hasa sisi vijana tunao wajibu wa kuyatekeleza kwa vitendo mambo mema ya Mwalimu," alisema.

"Mwalimu alikuwa mzalendo, hakupenda rushwa na ufisadi, alipenda haki, na sisi tunapaswa kumuenzi Mwl.Nyerere kwa kuyatekeleza hayo" alisema Mtaka.

Akiwa Mkoani Simiyu Balozi Amina alitembelea viwanda vidogo na vya kati vikiwemo kiwanda cha chaki (Maswa) na cha kusindika Maziwa(Meatu) pamoja na maeneo ya wawekezaji katika mazao ya biashara (Pamba) na chakula (mchele).

Mhe.Waziri amehitimisha ziara yake mkoani Simiyu kwa kuihakikishia Serikali ya Mkoa huo kuwa Zanzibar iko tayari kufanya biashara na mkoa huo kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla, jambo lililoungwa mkono na viongozi wa mkoa huyo.

Comments

Popular posts from this blog

JUHUDI ZA MWALIMU NYERERE KATIKA KUKUZA NA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII NCHINI