Kamati ya GFT yakagua maendeleo ya Mradi wa JNHPP, yaipongeza serikali
Kamati ya Uwezeshaji ya Mradi wa kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP), kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali (GFT) imeipongeza serikali kwa kupiga hatua zaidi katika utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo.
Pongezi hizo zimetolewa na Meneja Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TAZARA) Mhandisi Fuad Abdallah kwa niaba ya wajumbe wote wa GFT wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo inayofanyika katika maeneo tofauti ya mradi huo, kuanzia June 6-11, mkoani Pwani.
Mhandisi Fuad alisema kuwa wamefanya ziara hiyo kwa kukagua maeneo mbalimbali ya mradi huo ambapo walikagua maendeleo ya ujenzi wa Tuta kuu la Bwawa, Kituo cha Kuchochea Umeme, Nyumba ya kuendeshea Mitambo ya kuzalisha umeme na Kingo za Bwawa (Saddle Dam)
Comments
Post a Comment