WIZARA YASAINI MAKUBALIANO NA KAMPUNI YA EXTENSIA YA UINGEREZA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect, tukio lililofanyika  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (katikati) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakitia saini Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect. Anayeshuhudia kulia ni Mkurugenzi wa Sheria wa Wizara hiyo, Bi. Lugano Rwetaka. 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akibadilishana nyaraka na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakati wa tukio la utiaji saini wa Mkataba wa Makubaliano wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi (Kulia) na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik wakionesha nyaraka zilizosainiwa za Makubaliano baina ya Wizara na Kampuni hiyo ya kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect  Julai 25, 2022 jijini Dodoma.

 


Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Jim Yonazi akizungumza baada ya kusaini Mkataba wa Makubaliano na  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, Bw. Tariq Malik (kushoto) wenye lengo la kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect   Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, Bw. Tariq Malik akizungumza wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa makubaliano baina ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Tewknolojia ya Habari na Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza  Julai 25, 2022 jijini Dodoma 


Picha ya pamoja ya baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Jim Yonazi (wa nne kushoto mstari wa mbele) na watendaji kutoka Kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Kampunihiyo, Bw. Tariq Malik (wanne kulia mstari wa mbele kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano baina ya Wizara na Kampuni hiyo wa kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect   Julai 25, 2022 jijini Dodoma.


 Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesaini mkataba wa makubaliano na kampuni ya Extensia Limited ya Uingereza, lengo likiwa ni kuandaa Kongamano litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano wa ndani na nje ya nchi linalojulikana kama Connect To Connect.

 

Kongamano hilo pia linalenga kuzidi kukuza matumizi ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kufungua wigo wa mifumo, ubunifu na uwekezaji katika TEHAMA.

 

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Jim Yonazi amesema  Kongamano la Connect To Connect (C2C) litafanyika kwa siku mbili tarehe 7 na 8 Septemba, 2022 ambapo nchi nyingi zinatarajiwa kushiriki ikiwa ni pamoja na nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki.

 

Amesema kuwa Tanzania inaunganisha nchi saba za jirani ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Malawi, Zambia na Msumbiji  kupitia Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo kuwa na fursa kubwa ya kupeleka huduma na kuchichimua uchumi kupitia TEHAMA.

 

Dkt. Yonazi ameeleza kuwa Kongamano litatoa pia fursa kwa nchi zitakazoshiriki kufanya majadiliano, kujifunza na kuweka mikakati ya teknolojia ya habari na mawasiliano katika kuchangia uchumi , kuongeza fursa za uwekezaji, ajira na elimu.

 

Naye Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Extensia Limited, Bw. Tariq Malik amesema kuwa 

Kongamano hilo lilifanyika Tanzania kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2013 hadi 2015 na kuleta mafanikio makubwa. Aidha, Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Kongamano kwa mara nyingine ambapo itapaisha zaidi Tanzania kama kitovu cha mawasiliano. 

 

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Bw. Mulembwa Munaku amesema kuwa utiaji saini wa makubaliano hayo ni hatua ya awali ya kuanza maandalizi ya Kongamano kubwa litakalowakutanisha wadau wa sekta ya mawasiliano zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi.

 

Naye Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Habari- MAELEZO,Bw. Gerson Msigwa ameipongeza Wizara kwa juhudi za kuweka mifumo imara ambayo itasaidia kutimiza malengo ya Serikali ya kuinua uchumi wa nchi kupitia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

Comments

Popular posts from this blog

JUHUDI ZA MWALIMU NYERERE KATIKA KUKUZA NA KUIMARISHA SEKTA YA UTALII NCHINI